Chaguo La Chelsea na United katika Dirisha La Usajili

[Picha:Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Mpaka Sasa katika zile timu 6 kubwa katika Ligi kuu ya EPL ni timu mbili tu ambazo hazijafanya usajili wowote lakini Kuna tetesi za timu hizo kutaka baadhi ya wachezaji ambao wengine wanaonesha kutokuwa na Nia ya kujiunga na baadhi ya timu hizo. Manchester United pamoja na Chelsea ni timu zilizokubali baadhi ya wachezaji wake waondoke katika klabu hizo lakini wao mpaka Sasa Hakuna usajili walioufanya, Ila Kuna baadhi ya wachezaji wanaotakiwa kujiunga na timu hizo ambao ni wafuatao.

Raheem Sterling

Ikiwa bado haijawa rasmi kwa Muiingereza anayechezea timu ya Manchester City Raheem Sterling kuhamia Chelsea baada ya kudumu katika klabu hiyo kwa takribani miaka 7, Sasa mshambuliaji huyo wa Manchester City Raheem Sterling amekuwa mawindoni na timu ya Chelsea ambayo iko mbioni kusaka huduma yake katika msimu huu. Chelsea inasemekana iko tayari kutoa kitita Cha Paundi milioni 35 ili kumsajili Sterling lakini City wao wanahitaji dau la Paundi milioni 60 na kumuuza Sterling. Sterling anaweza kuwa mchezaji anayetarajiwa kuziba pengingo la Lukaku anayehamia Inter Milan kwa mkopo.

Ousmane Dembele

Ikiwa umebaki muda mchache kwa winga wa Barcelona na mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Ufaransa mkataba wake uisha akiwa na timu hiyo ya La liga katika majira haya ya joto, Sasa Ousmane Dembele amekataa kuongeza mkataba na timu hiyo ya Barcelona mpaka Sasa na Chelsea inasemekana kutaka kumpata mshambuliaji huyo katika msimu. Ukiachana na Chelsea pia PSG bado hawajakata tamaa ya kuisaka huduma ya mshambuliaji huyo.

Soma pia: Sababu Za Haaland Kujiunga Na Manchester City

Presnel Kimpembe

Ukiwa bado mkataba wake na PSG bado haujaisha mpaka 2024, Chelsea inasemekana kumtaka mchezaji huyo katika kuboresha safu yake ya ulinzi katika msimu ujao na pia ukaribu wa Kimpembe pamoja na Thiego Silva unasemekana kuweza kuleta tumaini kwa Chelsea la kumpata mchezaji huyo wa PSG na kuungana na kocha wake Thomas Tuchel waliyodumu na timu hiyo kwa miaka ya nyuma Mpaka Sasa Hakuna dau lililotajwa wazi katika kumsaini mchezaji huyo.

Christian Erikson

Akiwa ni kiungo mshambuliaji wa timu ya Brentford pamoja na timu ya Taifa ya Denmark, Christian Erickson (30) amekuwa moja ya wachezaji wanaowindwa na Manchester United baada ya Ten Hag kuonesha kuhitaji huduma yake ili kuboresha kikosi hicho Cha United. Kiungo huyo mshambuliaji amewekwa katika orodha ya United ikiwa ni muda mchache tu umebaki ili mkataba wake dhidi ya Brentford kuisha. Kuachana na United pia Tottenham Hotspurs ni timu nyingine inayo muwinda mchezaji huyo.

Frenkie De Jong

Barcelona wako tayari kuachana na mshambuliaji wao huyo katika majira haya ya joto na Manchester United wameonesha Nia ya dhati kabisa ya kumsajili De Jong (25), lakini kwa upande wake de Jong yeye hayuko tayari kuondoka katika klabu hiyo ya soka huku Erik Ten Hag akitaka kuungana na kijana wake huyo aliyekuwa naye Ajax katika misimu ya nyuma. Manchester United wako tayari kutoa dau La Euro milioni 70-80 ili kumpata De Jong kwa msimu huu.

 

Leave your comment