Sababu Za Haaland Kujiunga Na Manchester City

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Akiwa Kama mfungaji namba 3 katika Ligi ya Ujerumani kwa kuweka kambani jumla ya mabao 22 katika mechi 24 alizocheza huko Bundesliga Sasa Erling Haaland mshambuliaji aliyekua akiichezea Borussia Dortmund ameamua kukata shauri na kuhamia huko EPL akiwa na timu ya Manchester City ya Uingereza.

Zituatazo ni sababu 5 zilizomfanya Haaland kuondoka Bundesliga na kujiunga EPL alizozitoa wakati wa mahojianao akiwa katika viunga vya Etihad stadium.

Historia ya kusakata kabumbu katika familia yake

Akiwa ametokea katika familia ya soka baada ya Alfie Haaland ambaye ni  baba yake mzazi kusakata kabumbu huko miaka ya nyuma katika klabu hiyo ya Manchester City, Erling Haaland amaamua kurudi Tena Manchester City kutokana na sababu ya baba yake kuwa ni moja ya wachezaji wa klabu hiyo hivyo na yeye angependa kuwa moja ya wanafamilia watakaopita katika klabu hiyo ya soka ya huko Uingereza.

Pengine yaweza kuwa mapenzi makubwa ya Haaland baada ya kuwa Manchester City ndiyo timu yake ya kwanza katika Soka aliyoanza kuishabikia kipindi baba yake alipokuwa moja ya wachezaji wa timu hiyo.

Download FREE DJ Mixes on Mdundo

Ushawishi wa baadhi ya wachezaji kutokea Manchester City

Katika mahojiano hayo na mmoja wa waandishi wa habari wa ndani na Manchester City, Haaland alisema kuwa Kuna baadhi ya wachezaji waliomshawishi kujiunga na klabu hiyo ya soka, na moja ya wachezaji hao ni Riyad Mahrez ambaye alimwaga sifa nyingi juu ya klabu hiyo ya soka kwa Haaland ili aweze kukubali usajili na kuwa moja ya wachezaji wa City.

Kupendezwa na mtindo wa uchezaji Mpira wa Manchester City

Baada ya kuwa moja Kati ya mashabiki na watazamaji wa mechi za Manchester City Haaland ameonesha kupendezwa na jinsi timu hiyo inavyosakata kabumbu ikiwa uwanjani. Hii pia imemfanya mchezaji huyo kuongeza matamanio ya kuwa moja ya wachezaji wa Manchester City. Haya ameyasema wakati akihojiwa na mtangazaji huyo wa Manchester City na kusema "Naupenda mtindo huo, napenda mtindo wa mpira wa miguu wa kushambulia, wakati City wanacheza mpira ni kitu ninachokipenda zaidi."

Matamanio yake ya kuongeza kipaji chake akiwa chini ya Kocha Pep Guardiola

Haaland ameonesha tumaini lake akiwa chini ya Kocha wa City na kusema kuwa kutokana na yeye kujiunga na timu kubwa kama Manchester City anahisi atazidi kukua na kuwa Bora zaidi na hata Kasi yake ya ufungaji itaongezeka kwa kuwa na mabao mengi zaidi baada ya yeye kujiunga na Manchester City.

Ushabiki wake kwa Timu ya Manchester City

Licha ya kuwa Erling Haaland ni raia wa Norway lakini alizaliwa Uingereza huko Leeds na hii ni kutokana na sababu ya kuwa na makazi huko wakati baba yake akiwa mchezaji wa City. Haaland alisema "Nimekuwa shabiki wa City maisha yangu yote" na hii ni kwa sababu ya kukua akiwa amezungukwa na maisha ya klabu hiyo ya soka.

Leave your comment