Antonio Rudiger aihama Chelsea Ajiunga na Miamba ya La liga

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Baada ya kukataa kuongeza mkataba na Chelsea Sasa Basi, habari zilizopo ni kuhusiana na Antonio Rudriger beki wa Kati wa Chelsea kujiunga na Real Madrid kwa mkataba utakaodumu kwa takribani miaka minne huko Santiago bernabeu akiwa Kama mchezaji huru.

Toni ambaye alijiunga na wababe hao wa Stanford bridge mnamo mwaka 2017 kutokea Roma na alisajiliwa kwa jumla ya Euro milioni 29 katika msimu wa mwaka huo.

Soma Pia: Paul Pogba Kuihama Manchester United

Mchezaji huyo wa timu ya Taifa ya Ujerumani inasemekana anatarajiwa kulipwa kiasi cha Euro 340,000 kwa wiki akiwa katika viunga hivyo vya Bernabeu lakini pia mwaka 2021 Chelsea walijaribu kusaka saini ya mchezaji huyo wa safu ya ulinzi mnamo mwezi wa 8 na kutakiwa kulipwa kiasi cha Euro 140,000 lakini alitupilia mbali dili hilo.

Katika kipindi chote ambacho ameichezea Chelsea ni jumla ya michezo 203 amewahi kuicheza timu hiyo na katika michezo hiyo ameweka magoli 12 kambani na pia katika kipindi hicho ambacho Yuko na Chelsea ameweza kushinda mataji mbalimbali Kama vile Uefa Champions League, Club world Cup, Europa league pamoja na FA Cup.

Rudriger ambaye amechagua kujiunga na miamba hao wa La liga na pia Ligi ya mabingwa Ulaya alikuwa Yuko mawindoni, akiwindwa na timu nyingi ikiwemo PSG,AC Milan, Manchester United, pamoja na Juventus.

 

Leave your comment