Paul Pogba Kuihama Manchester United
3 June 2022
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Stellah Julius
Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani ya Mdundo
Kiungo wa Timu ya Manchester United Paul Pogba anatarajiwa kuondoka katika viunga vya timu hiyo kama mcheziji huru baada ya mkataba wake kuisha na mashetani hao wekundu mwishoni mwa mwezi huu wa Juni.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anatarajiwa kufunga virago vyake baada ya kudumu na timu hiyo tangu msimu wa mwaka 2016/17 baada ya kusajiliwa kutoka Juventus kwa jumla ya Euro milioni 89 na kuleta gumzo.
Pogba ambaye pia ni kiungo wa Timu ya Taifa ya Ufaransa aliyeweza kuichezea timu hiyo ya Manchester United tangu kipindi alipokuwa na umri wa miaka 16 tu katika Academy ya United akitokea Le Havre pia alishawahi kuondoka United akiwa mchezaji huru na kujiunga na Juventus katika msimu wa mwaka 2012-2013.
Soma Pia: Historia Fupi ya Jose Mourhino Katika Soka "The Special One"
Katika academy hiyo ya Manchester United Pogba aliitendea timu hiyo kazi na kupata ushindi wa Kombe la vijana (Youth Cup) mnamo mwaka 2011 na pia Silverware kabla ya kuondoka klabuni hapo ilipofika mwaka 2012 na kuamua kujiunga na Juventus ya huko Serie A kabla ya kurudi Tena Old Trafford.
Baada ya kushinda mataji makubwa 8 akiwa Serie A, Mchezaji huyo aliyeiwezesha timu take ya Taifa ya Ufaransa kushinda kombe la dunia alionekana Kuwa mchezaji atakayeweza kuleta mabadiliko Kama akirejea Manchester United ndipo akasajiliwa, na katika mechi 233 alizocheza akiwa na United ameweza kufunga mabao 39 na kushinda ubingwa wa Carabao Cup pamoja na Kombe la Europa akiwa na timu hiyo.
Pogba pia alishawahi kuwa Captain msaidizi wa timu hiyo kabla ya kuwa na mtafaruko na kocha wa kipindi hicho Jose Mourinho akiwa klabuni hapo
Katika timu hiyo ya United si tu Paul Pogba anayetarajiwa kuondoka katika klabu hiyo, wachezaji wengine ni kama vile Juan Mata,Edinson Cavani, Nemanja Matic, Lee Grant, Jesse Lingard anayetarajiwa kukipiga West Ham.
Leave your comment