Historia Fupi ya Jose Mourhino Katika Soka "The Special One"

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Kama kuna kitu ambacho kimepelekea José Mourinho awe ni "Special One" ukiachana na ubishi pamoja na Tambo zake ni utashi na rekodi alizoziweka na kuweza kufundisha Ligi kubwa nne duniani ambazo ni English Premier League ya Uingereza, Serie A ya Italia, Primeira Liga ya Ureno pamoja na  La Liga ya Hispania ambazo Ligi zote hizi ameweza kuleta changamoto, ushindani hata kwa timu pinzani katika Ligi hizo na ubingwa katika timu alizofundisha

Safari Yake ya Ukocha

Mreno huyo mwenye umri wa miaka 59 alianza kazi ya ukocha mwaka 2000 kwenye klabu ya Benfica ya huko nchini Ureno, wasifu wake ulizidi kung'aa alipojiunga na FC Porto mwaka 2002 kisha kutimkia darajani mwaka 2004 ambapo alihudumu kwa misimu mitatu.

Baada ya kushinda Ligi ya mabingwa akiwa na timu ya Inter Milan, ilipofika mwaka 2010 Mourinho alielekea Real Madrid ambapo alifundisha kwa misimu mitatu. Timu nyingine ambazo The Special One amefundisha ni pamoja na Manchester United ambapo baada ya kufika Old Trafford, Mourinho aliweza kuleta tumaini jipya kwenye timu hiyo kufuatia kuondoka kwa Sir Alex Ferguson.

Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com

Kuvunja Rekodi

Licha ya kuwa ni kocha mwenye uzoefu mkubwa pamoja na ujuzi mwingi,pia Mourinho ameweza kuvunja rekodi baada ya kushinda ubingwa wa Uefa Europa Conference league akiwa na Ac Roma ya Italia kwa msimu wa mwaka 2021-2022 na ni baada ya kudumu na timu hiyo kwa miezi 11 tu mpaka Sasa ni ikiwa ni ubingwa wake wa 5 mkubwa kushinda katika Ligi za Ulaya.

Mataji Aliyoyapata katika ligi za mabingwa na shirikisho

Kwa ushindi Alioupata akiwa na Ac Roma katika Uefa Europa Conference league katika msimu huu kunamfanya Kocha huyo avunje rekodi kwa kushinda mataji makubwa 5 ya Ulaya akiwa na timu mbalimbali Kama vile FC Porto  pamoja na Inter-milan aliposhinda UEFA Champions 2004 na 2010, Europa league akiwa na Manchester United katika msimu wa mwaka 2016-2017 na mwaka 2003 akiwa na FC Porto alishinda ubingwa wa Uefa Cup ambao huu ukiwa ndio ubingwa wake wa kwanza mkubwa kuwahi kushinda barani Ulaya.

Timu aliyoisimamia bila kupata ubingwa wowote

Tottenham Hotspurs ni timu nyingine ambayo Mourinho amefundisha   ambapo kwa mara ya kwanza Mourinho alishindwa kubeba taji lolote akiwa na timu hiyo baada ya kutimuliwa Manchester United na kupata mkataba na Spurs mwaka 2019 lakini 2021 aliondoka katika klabu hiyo bila ubingwa wowote.

Leave your comment