Uchambuzi Mechi ya Liverpool Vs Real Madrid-UCL

[Picha: telegraph.co.uk]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Ni katika uwanja wa Stade de France fainali za Mabingwa wa Ulaya zilipofanyika katika jiji la Paris siku ya Jumamosi,siku ambayo Liverpool ya Uingereza walipovaana na Real Madrid ya Uhispania  na dakika 90 zikakamilika na sauti zilizotamba kwa mawanda mapana kwa wakati huo ni HALLA MADRID.

Ni ubingwa wa 14 kwa vinara hao wa La Liga Real Madrid baada ya safari yao ya ubingwa waliopita kupambana na vibonde wa Uingereza kwani hatua ya robo fainali walimtoa bingwa mtetezi wa ubingwa huo Chelsea na nusu fainali walipopambana katika come back ya kibabe na hatimaye kumtoa Manchester City huku fainali walipokutana Tena na Liver na wao ndio waliowapa ubingwa kwa kutia kambani goli dakika ya 56, goli lililofungwa na Viniciur Jr kinda wa kibrazili baada ya kupata cross Makini Sana kutoka kwa Federico Valverde.

Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com

Katika mchezo huu Liver wao walikuwa wanatafuta ubingwa mbele ya Real Madrid Kama kulipiza kusasi Cha 2018 walipotolewa na Madrid 3-1 na pia Mo Salah akitolewa nje baada ya kupata majeraha ya bega.

Umiliki wa mpira 54% kwa liverpool na Real Madrid wakimiliki mpira kwa 46%, mashoti ya moja kwa moja golini Liver walipiga 9 lakini Real wakipiga 2, jumla ya Kona kwa Liver zilikuwa 6 huku Madrid wakipata Kona 2 tu.

Offside ilikuwa 1tu kwa Liverpool Ila Los Blancos wakipata offsides 4, kwa mlinda mlango wa Madrid Thibaut Courtoir aliisaidia mipira 9 isiingie golini huku Alison Baker hakusaidia mpira wowote kutokuingia golini. Kwa upande wa kadi ni kadi moja ya njano ndiyo kadi pekee ilitolewa mchezoni hapo kwa Farbinho mchezaji wa Liverpool.

Baada ya mchezo kuisha na Madrid kuchukua ubingwa kwa ushindi wa bao 1-0 umekuwa ubingwa wa 5 kwa wachezaji baadhi wa timu ya Madrid akiwemo Benzema,Casemiro, Tony Kroos, Gareth Bale pamoja na Luca Modric lakini pia kwa kocha wao Carlo Ancelotti naye pia ndio ubingwa wake wa nne kuupata wa UEFA akiwa kocha wa timu tofauti tofauti ikiwemo Ac Milani waliobeba ubingwa Mara mbili.

Kwa upande wa kocha wa Liverpool Jürgen Klopp yeye baada ya kukosa kombe hilo la UEFA amezungumza na vyombo vya habari na kusema wanajiandaa na msimu ujao wa UEFA huko Instanbul na kuangalia ni hoteli gani watafikia.

Leave your comment