Tundaman ft Harmonize 'Badman', Jay Melody ft Marioo 'Sugar' Remix na Nyimbo Zingine Zinazovuma Bongo Wiki Hii

[Picha: Facebook]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma za Maua Sama Bila Malipo Kwenye Mdundo

Kama kuna kitu ambacho kinachochea ushindani na ustawi kwenye muziki wa Bongo Fleva basi ni mtandao wa YouTube ambao mashabiki wengi wa muziki kutoka Tanzania hutumia jukwaa hilo kwa ajili ya kusikiliza muziki na kutazama video za wasanii wao wanaowapenda. 

Soma Pia: Maua Sama 'Cinema' EP, Hamisa Mobetto 'Yours Truly' EP na Nyimbo Zingine Mpya Bongo Wiki Hii

Kwa wiki hii, zifuatazo ni nyimbo 5 zinazotamba na kufanya vizuri zaidi kwenye mtandao wa YouTube Tanzania: 

Badman - Tundaman Ft Harmonize 

Wimbo wa 'Badman' kwa sasa unasikika kwenye kila kona ya Tanzania. Mashahiri mazuri pamoja na video yenye hadhi ya kimataifa vimechagiza kazi hii ambayo kufikia sasa imeshatazamwa mara laki tisa sabini na nane kwenye mtandao wa YouTube kuwa bora sana. 

https://www.youtube.com/watch?v=RS9PMaKJHQ4

Naogopa - Marioo Ft Harmonize 

Naogopa ya kwake Marioo akiwa amemshirikisha Harmonize imezidi kufanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube. Hii ni ngoma ambayo Marioo ametumia muda na juhudi nyingi sana kuitangazai na kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 3.7 kwenye mtandao wa YouTube. 

https://www.youtube.com/watch?v=LJONP5YAokU

Pakua Nyimbo za Marioo Bila Malipo Kwenye Mdundo

Sugar Remix - Jay Melody Ft Marioo

Ukweli ni kwamba ngoma ya Sugar Remix ya kwake Jay Melody na Marioo imepokelewa kwa uzuri na uzito uliostahili na mashabiki wa muziki kutoka Tanzania kwani tofauti na toleo la kwanza, Sugar Remix imenogeshwa zaidi na sauti nzuri na midondoko ya aina yake kutoka kwa Marioo. 

https://www.youtube.com/watch?v=XojdvTGoj7s

Dunia - Harmonize 

Kwa takriban wiki mbili wimbo wa Dunia wa kwake Harmonize umeendelea kushika kasi kwenye mtandao wa YouTube. Kufikia sasa video ya ngoma hiyo ambayo ni ngoma namba 9 kwenye albamu yake ya High School imeshatazamwa mara Milioni 3. 2 kwenye mtandao wa YouTube. 

https://www.youtube.com/watch?v=yKJVlADjpus

La la - Mimi Mars Ft Marioo

Baada ya ukimya wa miezi takriban sita, Mimi Mars ameachia ngoma yake mpya ya kuitwa 'La La' ambayo amemshirikisha Marioo ambaye bila shaka ameweza kuinogesha kazi hii na kuifanya iwe bora sana. 

https://www.youtube.com/watch?v=kdbxocDkioY

Leave your comment