Maua Sama 'Cinema' EP, Hamisa Mobetto 'Yours Truly' EP na Nyimbo Zingine Mpya Bongo Wiki Hii

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma za Maua Sama Bila Malipo Kwenye Mdundo

Bila shaka muziki wa Tanzania unazidi kukua siku baada ya siku na shukrani nyingi ziwaendee wasanii ambao mara kwa mara wamekuwa wakitoa ngoma mpya ili kuweza kustawisha muziki wa Bongo na kuufanya uweze kutambulika zaidi. Kama unatafuta orodha ya ngoma mpya kutoka Tanzania ili uweze kupanua maktaba yako ya kimuziki, basi hii ni kwa ajili yako. Zifuatazo ni ngoma 5 kutoka kwa wasanii wa Tanzania ambazo zimeachiwa kwa wiki hii:

Hasira - Nay Wa Mitego Ft Hamadai
Huu ni wimbo ambao Nay wa Mitego anagusia hali ya maisha ilivyo kwa sasa nchini ambapo anagusia mambo ya msingi kama mfumuko wa bei. Anatuma ujumbe kwa Rais Samia ili aweze kushughulikia mambo hayo.  Kiiitikio cha ngoma kimepambwa na Hamadai ambaye ameweza kunogesha kazi hii. 

https://www.youtube.com/watch?v=ND5YcTczhzc

Yours Truly (EP) - Hamisa Mobetto
Baada ya ukimya wa miezi takriban 10 kwenye kiwanda cha muziki, Hamisa amerudi na EP yake ya nyimbo sita ya kuitwa 'Yours Truly' ambayo ndani yake amemshirikisha Korede Bello kutoka Nigeria pamoja na Otile Brown kutokea nchini Kenya. Hii ni EP ya kwanza ya Hamisa na ameweza kufanya aina tofauti tofauti za muziki kama Baibuda, Bongo Fleva, Afro Pop na Singeli. 

https://www.youtube.com/watch?v=SJbSaXRBuxo

First Born ( Album) - Beka Flavour 
Beka Flavour ndani ya wiki hii aliburudisha mashabiki zake na albamu yake mpya ya kuitwa First Born ambayo imesheheni ngoma 15 akiwa ameshirikisha wasanii tofauti tofauti kama Barnaba, Linah, YaMoto Band, Young Lunya, Christian Bella na wengineo. Hii ni albamu ya kwanza kutoka kwa Beka Flavour na kufikia sasa inafanya vizuri sana. 

https://www.youtube.com/watch?v=6kSI39xM6n4

Kama Ujui Utajua - Platform ft Balaa MC 
Wapenzi wa muziki wa singeli wiki hii walilipuka kwa furaha baada ya Platform kuachia 'Kama Hujui Utajua' akiwa na Balaa Mc. Mashahiri yake mepesi yanaeleza namna ambavyo mwanaume amezama kwenye mapenzi kiasi cha kutotaka kusikia kitu chochote kibaya kuhusu mpenzi wake. 

https://www.youtube.com/watch?v=bLg5HwarcPE

Cinema (EP) - Maua Sama 
Kipaji cha Maua Sama kimezidi kung'aa na hii ni baada ya msanii huyo kuachia Cinema, EP ambayo imesheheni ngoma 7 za moto huku akiwa amewashirikisha wasanii wawili tu ambao ni Alikiba kwenye 'Nioneshe' pamoja na Jux kwenye 'Falling in Love'. 

https://www.youtube.com/watch?v=Jl4tK56y2Y4

Leave your comment