Ubashiri wa mechi ya Aston Villa Vs Burnley-Alhamis hii

[Picha: skysports.com]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Mara baada ya mechi ya Aston Villa dhidi ya Burnley kuahirishwa masaa machache kabla ya mechi hiyo mnamo mwezi wa 12 baada ya taarifa ya kuzidi kwa Visa vya Uviko-19 katika kikosi Cha Aston Villa. Sasa basi mechi hiyo itaenda kuchezwa alhamisi hii ili kukamilisha mzunguko wa 18 katika Ligi ya EPL katika uwanja wa Villa Park.

Katika mechi hii Burnley wanahitaji matokeo ya uhakika kwa maana ya alama 3 wakiwa alama moja nyuma ya Leeds United ambapo kwa utofauti huo Burnley wanauwezekano wa kushushwa daraja Ila wakishinda kiporo hiki na mechi moja iliyobaki Basi kunauwezekano wa kubaki Ligi kuu EPL.

Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com

Kwa mujibu wa kocha wa Aston Villa Steven Gerald ametoa taarif ya kuwa mlinda mlango wao Emiliano Martinez amepata majeraha Jumatano na hatoweza kushiriki mechi zilizobaki wakati akifanya mazoezi.Majeruhi wengine katika kikosi Cha Aston Villa ni pamoja na Ezri Konsa, Kortney Hause, Leon Balley bado ni majeruhi.

Burnley katika mchezo huu wanaenda kuucheza bila ya wachezaji wake muhimu watatu ambao wanamajeraha,taarifa hiyo imetolewa na bosi wa muda wa timu hiyo na kusema kuwa Ben Mee, James Rodriguez pamoja na James Tarkowsky ni majeruhi lakini pia Dale Stephens na Erik Pieters wamerejea baada ya kupona majeraha yao.

Mchezo huu ni mchezo wa kukata na shoka kwani Aston Villa wanaenda kuwania kubaki katika nafasi 10 za juu huku wao Burnley wao wanaenda kutafuta nafasi ya kushiriki mashindano ya EPL kwa msimu ujao hivyo Basi Odds za mechi kuisha kwa sare ni 3.55

Leave your comment