Marioo ft Harmonize ‘Naogopa’, Diamond ‘Wonder’ na Nyimbo Zingine Zinazotamba Bongo Wiki Hii

[Picha: Clouds Media]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Kwa mashabiki wengi wa muziki wa Bongo Fleva, mtandao wa YouTube umekuwa ni moja kati ya mitandao ambayo hupendelea kupita na kuperuzi ili kuweza kusikiliza na kutazama video za wasanii wao pendwa. Mara nyingi YouTube imekuwa ni kama mizani ya kuweza kupima ni ngoma gani ambayo inafanya vizuri zaidi kwa hapa nchini Tanzania.

Zifuatazo ni ngoma 5 kali ambazo zinatamba na kufanya vizuri sana kwenye mtandao wa YouTube kwa hapa nchini Tanzania:

Soma Pia: Mtasubiri ft Zuchu na Nyimbo Zingine za Diamond Platnumz Zilizofungiwa Tanzania

Naogopa - Marioo ft Harmonize

Mashairi mazuri pamoja na video yenye stori inayosisimua kutazama ni kati ya vitu vichache ambavyo vimechagiza video ya Naogopa ambayo imeongozwa na Director Kenny kutokea nchini Tanzania kufanya vizuri sana kwenye mtandao wa YouTube. Kufikia sasa ngoma hiyo imeshatazamwa mara milioni 2.4 kwenye mtandao huo.

https://www.youtube.com/watch?v=LJONP5YAokU

Dunia - Harmonize

Ukweli ni kwamba video ya Dunia imezidi kuonyesha ubunifu mkubwa ambao Harmonize mara nyingi huutumia kwenye video zake za muziki. Video hii inamuonesha Harmonize mpya ambaye anaimba kwa hisia kwenye maeneo ya nyikani na siku sita tu tangu kuachiwa kwake video hii imeshatazamwa mara Milioni 2 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=yKJVlADjpus

Sona - Diamond Platnumz ft Adekunle Gold

Huitaji ujuzi kufahamu kuwa TG Omori ametumia ubunifu mkubwa sana na ufundi wa hali ya juu kuisuka video ya Sona ya kwake Diamond Platnumz akimshirikisha Adenkule Gold. Hii ni video ya nne kutoka kwenye EP ya First Of All ya Diamond Platnumz na bila shaka imepokelewa vyema na mashabiki kwani kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 1.5 kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Tuzo za Muziki za MTV Afrika Kufanyika Tanzania Mwaka 2023

https://www.youtube.com/watch?v=zpSj2Z2tbOg

Wonder - Diamond Platnumz

Wonder ni video ambayo Diamond Platnumz anaamua kuleta utamaduni wa Nigeria kwa watu wa Afrika Mashariki. Uhalisia pamoja na uigizaji mzuri wa muigizaji Jide Kosoko kwenye video hii umepelekea kazi hii kuwa na hadhi ya nyota tano na kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 4.1 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=MiMPut0PjVw

Niamini - Hamadai ft Alikiba

Uzuri wa ngoma ya ‘Niamini’ ya kwake Hamadai na Alikiba upo kwenye mashairi pamoja na muingiliano mzuri wa sauti kati ya wasanii hao. Kufikia sasa ngoma hii imeshatazamwa mara laki tano sitini na tatu ikiwa ni siku 7 tu tangu kuachiwa kwake.

https://www.youtube.com/watch?v=PunTEG27y58

Leave your comment