Ubashiri mechi ya Norwich City Vs West Ham Jumapili hii

[Picha: 90min.com]

Mwanadishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Norwich City wanakwenda kukichapa dhidi ya West Ham United Jumapili hii ya Mei 8 katika uwanja wa Carrow Road Stadium huko Norwich City England ikiwa ni mchezo wa Ligi kuu England.

Norwich ambayo kwa Sasa inashika nafasi ya 20 inajiweka katika Hali ngumu ya kushuka daraja katika ligi hiyo wanavaana na West Ham ambao wako nafasi ya 7 ambayo kwa wao inawaweka katika eneo zuri la kushiriki Europa Conference league kwa msimu ujao.

Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com

Kocha wa Norwich Dean Smith alithibitisha katika mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya kucheza kwa West Ham United kuwa kwa upande wa majeruhi McLean amevunjika kidole cha mguu na atalazimika kuvaa kiatu cha kujikinga hivyo anauwezekano wa kushiriki katika mechi hiyo huku Sargent amezidisha jeraha lake la kifundo cha mguu na hataweza kushiriki katika mechi za msimu zilizosalia na hii inaowafanya waungane na Adam Idah na Andrew Omobamidele kutafuta kujitayarisha kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2022/23.

Christoph Zimmermann ataukosa mchezo wa West Ham kwani bado yuko nje na tatizo la paja.

Kwa upande wao the Hummers wao baada ya kuondolewa katika mashindano ya Europa league dhidi ya Frankfurt kwa Sasa wanaelekeza nguvu zao huko EPL, na kwa upande wa majeruhi West Ham wao wanauwezekano wa kumkosa Angelo Ogbonna mwenye majeraha katika maungio ya miguu na hatoweza kushiriki mechi zilizobaki mpaka msimu uishe.

Ikumbukwe tu Katika mechi 5 ambazo Norwich na West Ham United walikipiga ni mechi  3 West Ham alipata alama zote tatu na mechi 2 wakagawana alama

West Ham kushinda katika mechi hii amepewa odds za 1.75.

Leave your comment