Ubashiri mechi ya Leicester city Vs As Roma-Alhamisi hii

[Picha: Sportsbrief.com]

Mwanadishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

UEFA conference league inaendelea Tena ambapo Leicester City wakiwa nyumbani wanawakaribisha vijana wa Jose Mourinho katika uwanja wa King Power Stadium katika mzunguko wa kwanza wa nusu fainali hizo Alhamisi hii.

Fox ambao wako nafasi ya 10 Premier League, wanauwezo wa kubaki  Uefa Conference league Kama watabeba kombe Hilo kwani kwa nafasi aliyopo Premier League haiwaweki katika hatua nzuri  ya kufuzu mashindano makubwa ya Ulaya.

Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com

Leicester City katika mechi zao za hivi karibuni wameshindwa kuonesha makali yao kwa wamefungwa na Newcastle na kulazimishwa sare katika mechi mbili ya Aston Villa pamoja na ile ya Everton.

Vijana hao wa Brendan Rodgers wanatiwa nguvu na kurejea kwa Jamie Vardy, hata hivyo, mshambuliaji huyo akitokea benchi dhidi ya Aston Villa na kucheza mechi yake ya kwanza tangu mapema Machi alipopata majeraha ya goti.

Roma, wakati huo huo, walilazimishwa sare ya bao 1-1 na Napoli na kuchapwa na Inter-milan bao 3-1 na kuvunja rekodi yao ya kucheza mechi 12 bila kufungwa, lakini wanasalia katika nafasi ya tano kwenye Serie A na wako kwenye nafasi ya kucheza Ligi ya Europa, ingawa Fiorentina pamoja na Lazio wakiwafukuzia kwa ukaribu zaidi.

Mourinho anakutana na Leicester City akiwa Hana wachezaji wake kama kiungo Bryan Cristante pamoja na mshambuliaji wake Nicolo Zaniolo ambaye mapema hivi karibuni alishinda hat-trick dhidi ya FK Bodo Glimt ya Norway.

Kati ya timu Leicester City pamoja na AS Roma mshindi anaenda kuvaana na timu Kati ya Feyenoord au Marseille katika fainali za Uefa Conference league.

Odds zilizotolewa kwa mechi kuisha kwa sare ni 3.40

Leave your comment