Ubashiri Mechi Ya Liverpool Vs Manchester United kwenye Premier League  Jumanne Hii

[Picha: supersport.com]

Mwanadishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Jumanne ya EPL iliyojaa shauku ya kutaka kujua mwisho wa usiku wa Leo ni Nani anaenda kuongoza ligi kuu hiyo wakati 'Reds team' zinapokutana katika kusaka alama 3 muhimu sana kwao.

Katika uwanja wa Anfiel Majogoo wa London Liverpool wanapo wakaribisha mashetani wekundu Manchester United katika mechi ya ligi kuu hiyo EPL kuelekea mwishoni mwa msimu.

Katika mechi hii ushindi wa Liverpool utawafanya wawe kinara katika ligi hiyo na kuwashusha Manchester City katika nafasi ya kwanza waliyodumu kwa zaidi ya robo ya msimu

Free Download: Pakua Mixes kali ndani ya Mdundo

Huku wao United kushinda katika mechi hii kutawafanya wapande nafasi moja zaidi na kuwa nafasi ya 5 nyuma ya Tottenham Hotspurs walio nafasi ya 4.

Kwa sasa kila timu iko katika malengo yake, kwa upande wa Liverpool wao wanania ya kupata ubingwa wa EPL huku wao United Wana Nia ya kupanda nafasi zaidi ili waweza kuahiriki UEFA Champions League katika msimu ujao.

Sasa basi Liverpool wao wamekamilika katika kikosi Chao kwani mpaka Sasa wachezaji wake wote wako fiti Kali kitu katika kusakata kabumbu Usiku wa leo.

Lakini wao United wanawakosa wachezaji wake muhimu sana haswa katika mechi muhimu Kama hii, wachezaji hao ni Scott Mctominy, Edinson Cavan, Fred, Luke Shaw, pamoja na Raphaël Varane.

Liverpool wao wako Katika kiwango Bora zaidi kwani katika mechi 5 za nyuma wamepata ushindi katika mechi 3 na kudroo mechi 2.

Na wao United katika mechi 5 za nyuma wameshinda mechi 2, droo mechi 1 na wamepoteza mechi 2.

Je! katika mechi hii nyota wa United Cristiano Ronaldo ataweza kukipiga baada ya matatizo ya kifamilia?

Odds zilizotolewa kwa timu zote mbili kuona lango pa mwenzake ni 1.74

Leave your comment