Ubashiri Mechi Wa Bayern Munich Vs Villarreal Jumanne Usiku

[Picha: 90min.com]

Mwanadishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Mara baada ya kupata matokeo yenye kumbukumbu kwao kwenye mechi ya kwanza, Villarreal sasa nao wanafunga  safari kwenda kukutana na Bayern Munich katika mzunguko wa pili wa robo fainali za Ubingwa wa Ulaya usiku wa Jumanne hii.

The yellow submarine waliowabamiza Bayern Munich bao 1 kwa sifuri lililofungwa na Arnaut Danjuma,Sasa wanatakiwa waweza kuwachezesha Bayern Munich kwa akili ili waweze kufudhu nusu fainali.

Villarreal wao ndio walioanza kuwakaribisha Bayern katika uwanja wao wa nyumbani wa Ceremica na Sasa wanakwenda uwanja wa ugenini wa Allianz Arena ambao ndio uwanja wa nyumbani wa Bayern.

Pakua Qaswida Ya Mwezi ndani ya Mdundo

Bayern Munich wakiwa na mchezaji mwenye mabao mengi UEFA Robert Lewandowski mwenye mabao 12  wanahitaji mabao zaida ya moja na huku wao wakitakiwa kuhakikisha kuwa hawaruhusu bao lolote kutoka kwa Villarreal ambao wao tayari wanauhakika wa bao moja mbele yao.

Hii haitakuwa mechi rahisi kwa timu zote kwani Mara ya mwisho kwa Bayern Munich kushika ubingwa huo ilikua ni katika msimu wa mwaka 2019-2020 wao wakiwa na jumla ya mataji 6 ya UEFA na kwa Villarreal wao hawajawahi kushinda ubingwa huo wa UEFA.

The Bavari wao watawakosa wachezaji wake Kama Bouna Sarr, Niklas Süle, Lucas Hernández, Corentin Tolisso pamoja na Eric Maxim Choupo-Moting kwa kuwa ni majeruhi

Villarreal kwa upande wao wana majeruhi mmoja tu ambaye ni  kiungo wa kushoto wa kuitwa Alberto Moreno.

Baada ya mechi hii Kati ya Bayern Munich na Villarreal mshindi anakwenda kukutana na timu Kati ya Liverpool au Benfica katika nusu fainali.

Odds 10.50 ndizo alizowekewa Villarreal katika ushindi wa mechi hii.

Leave your comment