Tetesi Za Mbappe Za Kuongeza Mkataba na PSG

[Picha: Instagram]

Mwanadishi: Stellah Julius

Get football news and Prediction on Mdundo

Taarifa zilizopo mtandaoni kwa sasa ni kuhusu mshambuliaji wa timu ya Paris saint-Germain ya Ufaransa, Kylian Mbappe ambaye anasemekana kuwa yuko mbioni  kuongeza mkataba utakaodumu kwa miaka miwili kwa wenyeji hao wa Les Pare De Prince.

Mbappe alisajiliwa PSG kwa mkopo kutoka Monaco mwaka 2017, lakini baada ya kuonesha kiwango cha aina yake mwaka 2018 PSG walimsajili mazima kwa jumla ya Euro milioni 180 na kuwa mchezaji wa kudumu wa timu hiyo.

Mbappe mwenye umri wa miaka 23 kwa sasa ameonekana kunogewa sana na maisha ya PSG, kwani mwanzoni mwa mwaka huu alikataa dili aliyopewa na Real Madrid ya Hispania pamoja na kwamba Real Madrid ndiyo imekuwa timu ya ndoto zake.

Pakua Qaswida Ya Mwezi ndani ya Mdundo

Mkataba wa Mbappe dhidi ya PSG ulitarajiwa kuisha katika majira ya joto ya mwezi juni mwaka huu 2022 lakini winga huyo kaonesha kunogewa na timu yake hiyo kwa sasa.

Mkataba huu mpya anaotarajia kumwaga wino ili kuendelea kuchezea PSG unasemekana kugharimu Euro milioni 125 mpaka Euro milioni 150 na Mbappe baada ya mkataba huo atalipwa kiasi cha Euro milioni 40 kwa mwaka kama mshara

Mpaka sasa timu zilizokuwa mstari wa mbele katika kusaka saini ya winga huyo ni PSG ambao wanaonekana kutumia nguvu nyingi sana kumbakisha pamoja na Real Madrid ya huko nchini Hispania ambao wao walijihakikishia kuipata saini yake lakini siku za hivi karibuni wanaonekana kushindwa kufikia azma yao.

Timu nyingine zilizokuwa na ndoto ya kumsajili mfaransa huyo ni pamoja na Liverpool pamoja na Man City za Uingereza ambao kwa sasa wanaonekana kukata tamaa ya kumsajili  Kylian Mbappe.

Leave your comment