Ibraah ‘Rara’, Mac Voice ‘Sara’ na Nyimbo Zingine Mpya Bongo Wiki Hii
4 April 2022
[Picha: EATV]
Mwandishi: Charles Maganga
Free Download: Pakua Mixes 7 kali kutoka Tanzania za mziki wa Bongo, Singeli na Amapiano Tamu
Hii ni wiki ambayo wasanii tofauti tofauti wa Tanzania wameachia kazi mpya na bila shaka kama ungependa kutanua maktaba yako ya muziki kwa kusikiliza ngoma mpya kutokea nchini Tanzania basi umefika sehemu sahihi kabisa. Zifuatazo ni ngoma mpya 5 ambazo zimeachiwa na wasanii kutokea nchini Tanzania kwa wiki hii.
Pakua Ngoma zake Mac Voice Bila Malipo Kwenye Mdundo
Rara - Ibraah
Kutokea himaya ya Konde Gang, Ibraah amerudi baada ya ukimya miezi minne na ngoma yake mpya kabisa ya kuitwa Rara. Rara ni ngoma ambayo Ibraah anatoa sifa za kutosha kwa mpenzi wake. Kwenye kibao hiki Ibraah anaimba Bongo Fleva ambayo ni mchanganyiko wa Kiswahili pamoja na Kiingereza kinachotumia lahaja ya Nigeria ili kuweza kufikisha ujumbe wake. Video ya ngoma hii ambayo iliongozwa na Director Msafiri kutokea Kwetu Studios pia ilizidi kunogesha kazi hii ambayo kufikia sasa imeshatazamwa takriban mara Laki 9 kwenye mtandao wa YouTube.
Soma Pia: Nandy ‘Siwezi’, Diamond ‘Fine’ na Nyimbo Zingine Zinazovuma Bongo Wiki Hii
Sara - Mac Voice
Utakuwa umepitwa na mengi sana kama hujasikiliza ngoma mpya kabisa ya kuitwa Sara kutoka kwake Mac Voice. Ndani ya ngoma hii, Mac Voice anamsifia mwanamke aitwaye Sarah kwa kutaka awe mtu wake kimapenzi. Hii ni ngoma ambayo ndani yake Mac Voice ameonesha uwezo mkubwa wa kimuziki kwa kuweza kuimba lugha tatu yaani Kiswahili, Kiingereza na Kihispaniola kitu ambacho ni nadra sana kufanyika na msanii wa kitanzania. Video ya ngoma hii imeshatazamwa mara laki mbili kwenye mtandao wa YouTube.
Inatosha - Walter Chilambo ft Ambwene Mwasongwe
Wiki hii tasnia ya muziki wa Injili ilichangamshwa na video mpya kabisa ya wimbo wa Inatosha ambao ni ya kwake Walter Chilambo akiwa amemshirikisha Ambwene Mwasongwe ambaye ni moja kati ya wanamuziki wa Injili wanaoheshimika sana hapa Tanzania. Inatosha ni wimbo ambao Walter anatukuza ukuu wa Mungu kwani kupitia mashairi ya wimbo huu, Walter na Ambwene Mwasongwe wanashuhudia namna ambavyo Mwenyezi Mungu anawatosha na kuwabariki kwenye maisha yao ya kila siku. Hii ni moja kati ya collabo bora sana zilizowahi kutokea kwenye muziki wa Injili na kufikia sasa video hii imeshatazamwa mara laki moja kumi na tano kwenye mtandao wa YouTube.
Soma Pia: Diamond ft Zuchu ‘Mtasubiri’ na Collabo Zingine Bora Bongo Kutoka Januari hadi Machi 2022
I Miss You Mama - Lulu Diva
Pengine huu ndo wimbo wa maumivu na majonzi ambao Lulu Diva ameshawahi kuuachia tangu alipoingia rasmi kwenye kiwanda cha muziki miaka 6 nyuma. I Miss You Mama ni ujumbe wa Lulu Diva kwa mama yake mzazi ambaye alifariki miezi kadhaa nyuma. Kupitia ngoma hii, Lulu anaonesha jinsi ambavyo anatamani kumuona tena mama yake ambaye alikuwa kama Nguzo kwenye maisha yake.
Ma Everything - Kinata MC
Kinata MC amezidi kupeperusha bendera ya muziki wa singeli baada ya kuachia ngoma yake mpya kabisa ya kuitwa Ma Everything. Kinata MC bado anaendelea kuthibitishia umma kuwa inawezekana kabisa singeli ikaimbwa kwa lugha ya kiingereza na bila shaka hii ni ngoma ambayo itamuweka sehemu nzuri zaidi mtunzi huyu wa ngoma ya ‘Do Le Mi Go’ ambayo ilifanya vizuri.
Leave your comment