Nandy ‘Siwezi’, Diamond ‘Fine’ na Nyimbo Zingine Zinazovuma Bongo Wiki Hii
1 April 2022
[Picha: Ghetto Radio]
Mwandishi: Charles Maganga
Pakua Ngoma Zake Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo
Wiki ya kwanza kabisa ya mwezi Aprili umewadia na ushindani kwenye kiwanda cha muziki nchini Tanzania umezidi kunoga hasa kwenye mtandao wa YouTube ambako wasanii wengi hupendelea kupakia ngoma zao. Zifuatazo ni ngoma tano kutoka Tanzania ambazo zinafanya vizuri sana nchini Tanzania kwenye mtandao wa YouTube:
Free Download: Pakua Mixes 7 kali kutoka Tanzania za mziki wa Bongo, Singeli na Amapiano Tamu
Fine - Diamond Platnumz
Video ya Fine imezidi kufanya vizuri nchini Tanzania na shukrani nyingi sana zimuendee TG Omori ambaye alihakikisha video hii imeundwa na stori nzuri, mitindo bora ya kucheza, mtiririko mzuri wa matukio pamoja na ubora wa picha ambao ulikuwa ni wa kimataifa. Aidha, uamuzi wa Diamond Platnumz kuvaa nguo za kijeshi kwenye video hii uliibua hisia mbalimbali kwa mashabiki wa muziki nchini na Tanzania na kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 3.1 kwenye mtandao wa YouTube.
Mtasubiri - Diamond Platnumz ft Zuchu
Mtasubiri ni moja ya video iliyosubiriwa kwa hamu sana na mashabiki, na bila shaka Ivan ambaye ndiye ameongoza video hii alitendea haki subra za mashabiki kwa kutengeneza video bora sana. Mtasubiri kutoka kwa Diamond Platnumz imeweka rekodi ya kuwa video iliyofikisha watazamaji laki moja ndani ya muda mfupi zaidi Afrika baada ya kufikisha watazamaji laki moja ndani ya dakika 37 tu huku ikifikisha watazamaji Milioni 1 ndani ya saa 16 tu.
Siwezi - Nandy
Siwezi ya Nandy imeendelea kufanya vizuri nchini Tanzania na hii ni kutokana na namna ambavyo Nandy amekuwa mbunifu katika kuitangaza ngoma hii huku mashahiri pamoja na video ya ngoma hii vikiwa vimechagiza Siwezi kuzidi kufanya vizuri. Siku nane tangu kuachiwa kwake, Siwezi ya Nandy ambayo ndio ngoma yake ya kwanza kwa mwaka huu, imeweza kutazamwa mara Milioni 1.8 kwenye mtandao wa YouTube.
Nawaza - Diamond Platnumz
Ngoma ya Nawaza ya kwake Diamond Platnumz imezidi kuchanja mbuga huko YouTube kwani kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 3.3 kwenye mtandao huo ikiwa ni ngoma ya pili iliyotazamwa zaidi YouTube kutoka kwenye EP yake ya FOA, ya kwanza ikiwa ni Mtasubiri. Hii ni ngoma ambayo Diamond Platnumz amegusia maisha yake binafsi, maadui zake, washindani wake wa kimuziki na mambo mengine yanayomhusu.
Bakhresa - Harmonize
Ngoma ya Bakhresa imezidi kudhihirisha uwezo wa Harmonize wa kuandika ngoma zenye ujumbe tofauti tofauti ukiachana na mapenzi. Ngoma hii imeweza kupokelewa kwa mikono na mashabiki wa muziki nchini Tanzania. Kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 4.7 kwenye mtandao wa YouTube zikiwa zimeshatimia takriban siku 11 tu tangu kuachiwa kwake.
Leave your comment