Diamond ft Zuchu ‘Mtasubiri’ na Collabo Zingine Bora Bongo Kutoka Januari hadi Machi 2022

[Picha: Ghetto Radio]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Marioo bila Malipo kwenye Mdundo

Ukiweka kando matamasha ya kimuziki, albamu, EP pamoja na tuzo za muziki, kitu kingine kilichopamba kiwanda cha Bongo Fleva kwa mwaka huu ni pale ambapo wasanii wetu pendwa waliamua kuunganisha nguvu na kufanya nyimbo za pamoja kwa maana ya collabo.

Pakua Nyimbo za Jux Bila Malipo Kwenye Mdundo

Tukiwa tumeshafikia ukingoni kabisa mwa mwezi Machi, zifuatazo ni collabo 5 bora kwa mwaka huu kutoka kwa wasanii wa Tanzania:

Soma Pia: Free Download: Pakua Mixes 7 kali kutoka Tanzania za mziki wa Bongo, Singeli na Amapiano Tamu

Omoyo Remix - Harmonize & Jane Miso

Kwenye Omoyo Remix, Harmonize ameonesha uwezo wake wa kubadilisha wimbo wa zamani na kuufanya kuwa mpya kabisa. Video ya wimbo huu ambayo iliundwa na stori nzuri na ya kusisimia ilizidi kunogesha kazi hii ambayo kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 2.8 kwenye mtandao wa Youtube.

https://www.youtube.com/watch?v=Luj_vFdImVs

I Love You - Jux ft Gyakie

Jux mwezi Februari aliachia ngoma ya I Love You akimshirikisha Gyakie kutokea Ghana kama zawadi ya Valentine kwa mashabiki zake ambao mara nyingi huwa wanapagawa kwa nyimbo zake. Pamoja na kwamba ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuachia ngoma na msanii kutokea Ghana, Jux alionesha umahiri wake wa sauti na kimashahiri kwenye ngoma hii ambayo ilitayarishwa na Fox Made It, nguli wa, muziki kutokea Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=2ELyg7GZDQE

Mtasubiri - Diamod Platnumz ft Zuchu

Kutoka kwenye EP yake ya kuitwa First Of All, Mtasubiri ni ngoma ya kwanza ndani ya takriban miaka minne ambayo Diamond Platnumz amemshirikisha msanii wa kike.Hii ndio maana collabo hii ukiachana na ujumbe wake mzuri pamoja na mashahiri ya kusisimua ilizidi kupendwa sana na mashabiki wa muziki. Aidha, video ya Mtasubiri imeweka rekodi ya kuwa video ya muziki iliyofikisha watazamaji laki moja kwa haraka zaidi Afrika baada ya kufikisha watazamaji laki moja ndani ya dakika 37 tu huko kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=IokCG2J-_5Q

I Miss You - Rayvanny ft Zuchu

Collabo hii iligusa wengi ambao walishaachana na wapenzi wao lakini kwa sasa wanawahitaji tena kwenye maisha yao. Kama ambavyo walifanya kwenye ‘My Number One’, wimbo huu umejengwa na mashahiri mazuri na ya kuchoma hisia pamoja na mdundo mzuri kutoka kwa Lizer Classic ambao ulinogesha zaidi kibao hiki. Ngoma hii bado haina video ila kufikia sasa imepata mafanikio makubwa ikiwemo kutazamwa mara Milioni 2.5 kwenye mtandao wa YouTube miezi miwili tu tangu kuachiwa kwake.

https://www.youtube.com/watch?v=T69CmY6Kc5g

Yeeh - Moni Centrozone ft Marioo

Uwezo wa Marioo kuimba kwenye mdundo wa Hip-hop umedhihirika kwenye collabo hii matata ambayo ameshirikishwa na fundi wa rap kutokea Rooftop Entertainment, Moni Centrozone. Ikiwa ni siku chache tu tangu kuachiwa kwake, ngoma hii ambayo kufikia sasa video yake imeshatazamwa mara laki moja na elfu tisa inatarajiwa kufanya vizuri zaidi huko mbeleni kwenye mitandao mbalimbali ya kuuza na kusambaza muziki duniani.

https://www.youtube.com/watch?v=jISRfdmmraQ

Leave your comment