Diamond ‘Nawaza’: Watu 4 Maarufu Waliotajwa kwa Ngoma Hii Inayovuma Bongo

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Nyimbo za Ali Kiba Bila Malipo Kwenye Mdundo

Tangu aachie EP yake ya ‘First of All’, ngoma ya Nawaza imekuwa ni miongoni mwa ngoma bora kabisa kutoka kwenye EP hiyo ambayo imezidi kuimarisha jina la Diamond Platnumz kama mfalme wa Bongo Fleva.

Wimbo huu umependwa sana na wengi kutokana na namna ambavyo Diamond Platnumz ameweza kuongelea maisha yake binafsi, mwenendo wa tasnia ya muziki, washindani wake wake kimuziki na pia ameweza kuuliza maswali fikirishi ambayo ni ngumu sana kupata majibu.

Pakua Nyimbo za Vanessa Mdee Bila Malipo Kwenye Mdundo

Wafuatao ni watu wanne maarufu ambao wameweza kutajwa moja kwa moja au kwa mafumbo kwenye ngoma ya Nawaza.

Rayvanny

Kwenye aya ya kwanza Diamond Platnumz anaimba "Nawaza Vanny na Elizabeth, clip zao zikivuja. Ndoa itaimarika eti au ndo wataivunja." Mwezi Septemba mwaka 2019, kulikuwa na uvumi kuwa Rayvanny na muigizaji Elizabeth Michael wana mahusiano na hii ni baada ya Rayvanny kutumbuiza kwenye sherehe binafsi ya Elizabeth Michael.

Rayvanny alitoka hadharani kupiga madai hayo na kusema kuwa wao ni marafiki tu. Baada ya Nawaza kuachiwa, tetesi hizo zimeanza upya kwani mstari huu unaashiria kuwa kuna video za siri ambazo zinamhusu Rayvanny akiwa na mwanamke aitwaye Elizabeth ambaye wengi wamemtafsiri kama Elizabeth Michael kutokana na tetesi za kipindi cha nyuma.

Harmonize

Hakuna asiyejua kuwa kwa sasa Diamond Platnumz hana ukaribu tena na Harmonize. Hii ni baada ya Harmonize kujiondoa kwenye lebo ya WCB mwaka 2019 na tangu hapo, wawili hao wameonekana kuwa kwenye mgogoro. Mwezi Novemba mwaka 2021, Harmonize aliongea na waandishi wa habari kuhusu hasa chanzo cha yeye kuondoka WCB na aliainisha kuna baadhi ya fitna alifanyiwa kipindi anaondoka kwenye lebo hiyo kubwa Afrika Mashariki.

Kwenye ‘Nawaza’, Diamond Platnumz anaimba "Na nimejifunza binadamu kweli hawana jema, yaani mtoto unayemtunza ndo anakuombea ukilema." Wengi wametafsiri mstari huu kama ujumbe kwenda kwa Harmonize ambaye alitolewa na Diamond Platnumz mwaka 2015 lakini sasa hivi hawana mahusiano mazuri.

Ali Kiba

Kwenye aya ya kwanza Diamond Platnumz anasema “Nlowaza leo nshawaza sana mi na Kiba ugomvi kipi? Nikagundua ushamba, na ujana wa kugombania mashabiki." Kwenye mstari huu Diamond Platnumz anahoji nini hasa ni chanzo cha bifu lake yeye na bosi wa Kings Music Ali Kiba ambaye kwa miaka sasa wamekuwa wakishindanishwa kuhusu nani bora zaidi ya mwenzake.

Mstari huu unaashiria kuwa Diamond Platnumz aliamua kuachana kuendelea na bifu hilo dhidi ya Ali Kiba kwani anaona ni ushamba na njia ya kugombania mashabiki.

Mange Kimambi

Ingeshangaza sana kama ngoma hii ingekamilika bila Diamond Platnumz kumzungumzia mwanamitandao Mange Kimambi ambaye mara nyingi amekuwa akikosoa sana mtindo wa maisha ya Diamond Platnumz, ngoma zake na wanawake ambao Diamond Platnumz amekuwa nao kwenye mahusiano.

Diamond Platnumz anatumia aya ya kwanza kufikisha ujumbe wake kwa Mange Kimambi kwa kuimba "Nawaza kina Kimambi bwana wangekua wagawa ridhiki hivi kweli ningejulikana si wangenizima nsisikike." Huu ni ujumbe tosha kuwa Diamond Platnumz anaona mambo yanaoongelewa mtandaoni dhidi yake na kumfanya afikiri mbali sana.

https://www.youtube.com/watch?v=njxSViOtBbY

Leave your comment