Diamond, Harmonize Watawala Nyimbo Zinazovuma YouTube Tanzania Wiki Hii

[Picha: Citi Muzik]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Nyimbo za Vanessa Mdee Bila Malipo Kwenye Mdundo

Imekuwa ni wiki nzuri sana kwenye uwanja wa Bongo Fleva kwani mashabiki wa Tanzania wamezidi kuunga mkono ngoma kutoka kwa wasanii wao, huku wengi wao wakitumia mtandao wa YouTube kuweza kusikiliza muziki. Zifuatazo ni ngoma tano ambazo zinasikilizwa sana YouTube huku wasanii wawili ambao ni Diamond Platnumz pamoja Harmonize wakiwa ndio wasanii pekee wanaotawala orodha hii kupitia ngoma zifuatazo:

Pakua Nyimbo za Ali Kiba Bila Malipo Kwenye Mdundo

Nawaza - Diamond Platnumz

Kutoka kwenye EP yake ya First Of All, ‘Nawaza’ ni ngoma ambayo Diamond Platnumz anaimba kuhusu maisha yake ya kimuziki na familia huku akigusia bifu lake na Ali Kiba, kiwanda cha filamu Tanzania pamoja na vitu vingi ambavyo vimezidi kufanya ngoma hii kuwa bora sana.

https://www.youtube.com/watch?v=njxSViOtBbY

Mtasubiri - Diamond Platnumz ft Zuchu

Kama wewe ni mtumiaji mzuri wa Tiktok na Instagram, basi bila shaka utakuwa umeshasikia ngoma hii ya ‘Utasubiri’ ambayo ndani yake Diamond Platnumz na Zuchu wanaahidiana kupeana mahaba mazito huku wakiwarushia ‘madongo’ wale wote wasiopenda penzi lao kuwa.

https://www.youtube.com/watch?v=2WnDQnJ4UDY

Bakhresa - Harmonize

Kwenye ‘Bakhresa’, Harmonize anamsifia vilivyo Salim Ali Bakhresa ambaye ni mojawapo ya matajiri wakubwa hapa Tanzania kwa kuishi maisha binafsi bila kujikweza wala kujigamba. Wimbo huu umeweza kupokelewa kwa mikono miwili na mashabiki wa muziki Tanzania nzima kutokana na maudhui kuwa ya tofauti.

 https://www.youtube.com/watch?v=ZxcUiGHqINY

Oka - Diamond Platnumz ft Mbosso

‘Oka’ ni ngoma ambayo kwa sasa inatikisa sana kwenye sherehe na kumbi mbalimbali za starehe hapa nchini Tanzania kutokana na kuwa na mdundo wa kuchezeka pamoja na mashahiri shirikishi ambayo yatachagiza yeyote kucheza mara tu atakaposikia kibao hiki.

https://www.youtube.com/watch?v=H3VrQG9mtjM

Loyal - Diamond Platnumz

Kuvuma kwa ngoma hii kulianza mwaka jana baada ya Diamond Platnumz kuweka video fupi akiwa anaimba ngoma hii ya ‘Loyal’ huko Instagram . Hatimaye ikiwa imeshatimia miezi 9 tangu Diamond Platnumz aachie kionjo, ngoma hii imetoka rasmi na imeweza kufanya vizuri sana ndani ya muda mfupi sana.

https://www.youtube.com/watch?v=B6E5rvDzFYI

Leave your comment