Collabo Tano Zilizofanya Vizuri Kati ya Wasanii wa Tanzania na Nigeria

[Picha: Citi Muzik]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Nyimbo za Ali Kiba Bila Malipo Kwenye Mdundo

Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mwamko mkubwa kwa wasanii wa Tanzania kuupeleka muziki wa Bongo Fleva nje ya nchi. Moja kati ya mbinu ambazo wasanii hutumia ni kufanya collabo na wasanii wa mataifa mengine kando na Tanzania. Nigeria ni moja kati ya nchi ambazo wasanii wa Tanzania hupendelea sana kushirikisha wasanii wake.

Pakua Nyimbo za Vanessa Mdee Bila Malipo Kwenye Mdundo

Bila shaka ukiongea na wasanii kama Diamond Platnumz, AY, Harmonize na hata Vanessa Mdee watakubali kuwa, collabo ambazo wamefanya na wanigeria zimesaidia mno kupeleka Bongo Fleva kimataifa. Zifuatazo ni ngoma tano ambazo wasanii wa Tanzania walishirikisha wasanii wa Nigeria na kuweza kufanya vizuri:

Soma Pia: Diamond ‘Number one’, Alikiba ‘Aje’, Na Nyimbo Zingine Zilizopeleka Muziki Wa Bongo Fleva Kimataifa

Kisela - Vanessa Mdee

Hii ni ngoma ambayo Vanessa Mdee alimshirikisha Mr P ambaye mwanzoni alikuwa ni mshiriki kwenye kundi la P Square. Ngoma hii iliweka historia kwenye muziki wa Bongo haswa kutokana na video yake ambayo ilikuwa na stori ya tofauti sana na ya kuvutia na hivyo kuchagiza vituo vikubwa vya muziki barani Africa kama Soundcity, Trace na MTV Base kuipa nafasi. Aidha ngoma hii na P Square ilimfanya Vanessa Mdee kuwa msanii wa pili kutoka Tanzania kufanya kazi na director Clarence Peters kutoka Nigeria baada ya Diamond Platnumz kufanya hivyo 2014 kwenye video ya ‘My Number One Remix’.

https://www.youtube.com/watch?v=Cex_94XOLQA

Show Me What You Got - Harmonize ft Yemi Alade

Ngoma hii ya mwaka 2019 ilimfanya Harmonize kuwa msanii wa pili kutoka Tanzania kufanya kazi na Yemi Alade baada ya Diamond Platnumz. Hii ni ngoma ambayo ilichagiza sana Harmonize kujulikana huko nchini Nigeria kutokana na mdundo wake uliotayarishwa na Kriz Beatz kuwa wa kuchangamka. Kando na haya, Harmonize pia alionyesha uwezo mkubwa kwenye kuchanganya maneno ya kiswahili na lahaja ya kinigeria kwenye mashahiri, kitu ambacho kilivutia wengi.

https://www.youtube.com/watch?v=ePnIXt5T7e8

My Number One Remix - Diamond Platnumz ft Davido

Hii ni collabo ambayo ilipeleka muziki wa Bongo Fleva huko duniani na kwa mujibu wa Diamond Platnumz, ilikuwa ni almanusura tu afilisike wakati anaandaa collabo hii na Davido kwani alienda kukopa hadi kwenye mabenki ili aweze kumlipa Davido na kugharamikia video. Video ya ngoma hii ilifanyika huko Lagos nchini Nigeria na iliweza kumtambulisha vyema Diamond Platnumz huko Nigeria kwani miezi kadhaa aliweza kuteuliwa kuwania vipengele vitano kwenye tuzo za AFRIMA za mwaka 2015.

https://www.youtube.com/watch?v=Cd2bwLcgGGg

Bwana Mdogo - Ali Kiba ft Patoranking

Huitaji kuwa bwana mkubwa kujua kuwa, Bwana Mdogo ni moja kati ya collabo bora sana kutoka kwenye albamu ya Only One King ya kwake Ali Kiba. Collabo hii ilizidi kuchimba msingi wa Bongo Fleva huko nchini Nigeria kwani Patoranking ambaye ndiye ameshirikishwa kwenye ngoma hii alishiriki kikamilifu katika kuhakikisha ngoma inafahamika sana huko Nigeria.

https://www.youtube.com/watch?v=VvyDRDO6RLA

Kainama - Harmonize ft Diamond Platnumz & Burna Boy

Kutoka kwenye EP yake ya kuitwa Afro Bongo, Kainama ni wimbo ambao Harmonize amemshirikisha mshindi wa tuzo ya Grammy Burna Boy kutokea Nigeria. Huu ni wimbo ambao uliweza kupendwa sana kutokana na mitindo mizuri ya kuchezeka iliyoonekana kwenye video pamoja na ushirikiano mujarab ambao aliuonesha Harmonize, Diamond Platnumz na Burna Boy kwenye ngoma hii.

https://www.youtube.com/watch?v=teejx562wxg

Leave your comment