‘Harmonize ‘Bakhresa’, Diamond ‘First of All’ EP na Nyimbo Zingine Mpya Tanzania Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Pulse Live Kenya

Muziki wa Bongo Fleva unazidi kukua siku baada ya siku na hii ni kwa sababu kila wiki wasanii wakubwa kwa wadogo wamekuwa wakiachia ngoma mpya ambazo zimezidi kufanya Bongo Fleva kunoga zaidi. Zifuatazo ni ngoma tano kali ambazo wasanii kutoka Tanzania wameachia ndani ya wiki hii:

Pakua Nyimbo za Anjella Bila Malpo Kwenye Mdundo

Sokomoko - Abdu Kiba ft Maua Sama

Kwenye ngoma hii, Abdu Kiba na Maua Sama wanapashana maneno mazuri, wakiambiana ni kwa namna gani wanapendana sana huku wakituma ujumbe kwa maadui zao kuwa kamwe hawawezi kuwatenganisha.

https://www.youtube.com/watch?v=nqK7c1WyDt4

Bakhresa - Harmonize 

Hatimaye wiki hii Harmonize ameachia ngoma yake ya kuitwa Bakhresa ambayo ndani yake Konde Boy anamwaga sifa kedekede kwa Said Salim Bakhresa ambaye ni mojawapo ya matajiri wakubwa sana hapa nchini Tanzania. Kwenye kibao hiki kilichotayarishwa na Sign Beatz Harmonize anamsifia Bakhresa kwa mtindo wake wa kuishi maisha binafsi yasiyo na kujikweza.

https://www.youtube.com/watch?v=ZxcUiGHqINY

First Of All (FOA) EP - Diamond Platnumz

Baada ya subira ya muda mrefu hatimaye Diamond Platnumz aliweza kuachia EP yake mpya ya kuitwa First Of All ambayo imesheheni ngoma kumi, ikishirikisha wasanii kama Jay Willz, Adenkule Gold, Zuchu, Mbosso, Focalistic na wasanii wengine wengi. Kufikia sasa EP hii ambayo imetayarishwa na magwiji wa muziki Lizer Classic na S2kizzy imevunja rekodi mbalimbali za muziki hapa Tanzania kwenye mitandao mbalimbali ya kuuza muziki.

https://www.youtube.com/watch?v=2WnDQnJ4UDY

Soma Pia: Diamond ‘Kamata’, Harmonize ‘Happy Birthday’ na Nyimbo Zingine za Bongo Fleva Ambazo Huwezi kosa Kwenye Sherehe

Shulala - Anjella

Wiki hii mwanamuziki Anjella aliweza kuvunja ukimya baada ya kuachia ngoma yake ya Shulala ambayo ndani yake anasifia penzi na huba motomoto analopewa na mpenzi wake wa muda mrefu na kufikia sasa ngoma imeshatazamwa mara laki moja na elfu tano kwenye mtandao wa YouTube.

 https://www.youtube.com/watch?v=uRII-LpXt90

Mama Ntilie - Shilole

Kwenye ‘Mama Ntilie’, Shilole anaweka wazi namna ambavyo anafurahi kuona biashara yake ya chakula inazidi kukua huku baadhi ya mistari ya ngoma ikitafsiriwa na mashabiki kama jumbe kwa, mpenzi wake wa zamani Uchebe na msanii mwenzake Ali Kiba.

https://www.youtube.com/watch?v=obHCxvUOsr0

Leave your comment