Diamond ‘Kamata’, Harmonize ‘Happy Birthday’ na Nyimbo Zingine za Bongo Fleva Ambazo Huwezi kosa Kwenye Sherehe

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Nyimbo za Marioo Bila Malipo Kwenye Mdundo

Uzuri wa sherehe yoyote iwe harusi, sherehe ya kumbukizi ya kuzaliwa, mahafali au hata mtoko wa klabu, siku zote hunogeshwa zaidi na ngoma ambazo zitachezwa kwenye sherehe hiyo. Mara nyingi huwa kuna zile ngoma ambazo zikipigwa kwenye sherehe, mwili bila hiyana unajikuta unacheza na akili inafurahi.

Soma Pia: Zuchu ‘Sukari’, Vanessa Mdee ‘Closer’ na Nyimbo Zingine za Wasanii wa Kike Tanzania Zilizoweka Rekodi

Zifuatazo ni ngoma tano za Bongo Fleva ambazo ni maarufu sana kuchezwa kwenye sherehe mbalimbali hapa Tanzania:

Beer Tamu - Marioo

Kama uko klabu na sehemu yoyote ya starehe hasa nyakati za usiku basi ni lazima ngoma hii kutoka kwa Marioo ipigwe ili kuchangamsha watu. Ukiweka kando mdundo wake wa Amapiano, ujumbe wa kwamba pombe ni tamu mara nyingi uhamasisha wengi kucheza ngoma hii hasa wakiwa klabu.

https://www.youtube.com/watch?v=J5Ka53RZUtE

Happy Birthday – Harmonize

Huu ni wimbo ambao mpaka staa wa muziki kutoka Hollywood Lupita Nyong'o aliweza kuucheza siku chache zilizopita akiwa anaadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa kwake. Kwenye ‘Happy Birthday’, Harmonize anatumia sauti yake mujarab kuweza kumtakia heri mpenzi wake kwa kuweza kufikisha mwaka mwingine. Licha ya kuachiwa zaidi ya miaka mitano iliyopita, wimbo huu mara zote umekuwa ni wimbo pendwa pale watu wanapofanya sherehe za siku ya kuzaliwa.

https://www.youtube.com/watch?v=l9O_SFcH4Kk

Miss Buza - Rayvanny

Wimbo huu wenye mahadhi ya singeli ni maarufu sana kwenye sherehe ambazo hufanyika maeneo ya uswahilini. ‘Miss Buza’ mara nyingi husikika kwenye harusi za uswahilini almaarufu kama vigodoro kwa hapa Tanzania. Mara zote DJ anapoamua kuweka ngoma hii, wahudhuhuriaji huchanganyikiwa kwa furaha kutokana na mdundo wake kuwa wa kuchangamsha na pia mashahiri yake ambayo ni shirikishi na mepesi.

https://www.youtube.com/watch?v=0PWCMHTJRn4

Watakoma - Amber Lulu ft Country Wizzy

Huu ni wimbo ambao ni maalum kwa ajili ya mapumziko ya mwisho ya wiki hasa kwa wale watu ambao wanapendelea kwenda klabu na sehemu za starehe. Mashairi ya ngoma hii yanamuonesha Amber Lulu ambaye anakusanya marafiki zake na kuwapeleka klabu. Anapofika huko klabu, nakutana na Country Wizzy ambaye mistari yake kwenye wimbo huu inathibitisha kwanini ‘Watakoma’ ni wimbo maarufu sana kwenye klabu mbalimbali hapa Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=2I6LfQZoZiI

Kamata - Diamond Platnumz

Orodha hii ingekuwa batili kama ‘Kamata’ ya Diamond Platnumz ingekosekana. Huu ni wimbo ambao maDJ hupendelea kuutumia klabu ili kuhamasisha watu kucheza na kukamatana haswa pale wanapokuwa klabu. Namna ambavyo Diamond Platnumz aliweza kutoa maelekezo ya jinsi watu wacheze kwa mtindo fulani, ni kitu ambacho kimepelekea ngoma hii kuwa kama sukari kwenye klabu mbalimbali hapa nchini Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=0dtdfKEoMuU

Leave your comment