Nyimbo Mpya: Diamond Platnumz Aachia ‘First Of All’ (FOA) EP

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Staa wa muziki kutokea nchini Tanzania Diamond Platnumz ameachia EP yake mpya  ya kuitwa First Of All (FOA) ambayo imekuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa.

Soma Pia: Diamond ‘Kamata’, Harmonize ‘Happy Birthday’ na Nyimbo Zingine za Bongo Fleva Ambazo Huwezi kosa Kwenye Sherehe

First Of All ni EP ambayo imesheheni ngoma 10 za moto na ndani yake Diamond Platnumz ameshirikisha wasanii tofauti tofauti kama Mbosso na Zuchu kutokea Tanzania, Jay Willz na Adenkule Gold kutokea Nigeria pamoja na Focalistic, Costa Titch na Pabi Cooper kutokea Afrika Kusini.

Aidha kazi hii yenye hadhi ya kimataifa imetayarishwa na watayarishaji wakubwa wa muziki ikiwemo S2kizzy, Krizbeatz, Sugavybz pamoja na Lizer Classic ambaye pia amehusika kwenye maandalizi ya mwisho kabisa ya kazi.

Ikumbukwe kuwa hii ni EP ya kwanza kutoka kwa Diamond Platnumz na inakuja kama matayarisho ya msanii huyo kuachia albamu yake mpya ambayo inatarajiwa kutoka baadaye mwakani.

Tayari imeshatimia miaka mitano tangu Diamond Platnumz aachie albamu yake ya kuitwa ‘A Boy From Tandale’ ambayo iliweza kufanya vizuri ndani na nje ya nchi.

Kwenye ‘A Boy From Tandale’ Diamond aliwashirikisha wasanii kama Rick Ross, Morgan Heritage, Omarion, Rayvanny na wasanii wengine wengi.

Ifuatayo ni orodha ya nyimbo kwenye EP mpya ya Diamond ‘First of All’:

  1. Melody ft Jaywillz
  2. Somebody
  3. Fine
  4. Mtasubiri ft. Zuchu
  5. Son aft. Adenkule Gold
  6. Loyal
  7. Wonder
  8. Nawaza
  9. Oka ft Mbosso
  10. Fresh ft Focalistic, Costa Titch & Pabi Cooper

Leave your comment