Harmonize ft Fik Fameica ‘Champino’ na Nyimbo Zingine Mpya Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii

[Picha: EATV]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Hakuna jambo jema kama kama kuanza wiki yako kwa kuongeza ngoma mpya kutoka kwa wasanii watanzania kwenye maktaba yako ya muziki. Zifuatazo ni ngoma tano mpya ambazo wasanii kutoka Tanzania wameachia ndani ya wiki hii:

Pakua Nyimbo Zake Nay wa Mitego Bila Malipo Kwenye Mdundo

Tumerogwa - Nay Wa Mitego

Utakuwa umepitwa sana kama bado hujasikiliza ngoma mpya kabisa kutoka kwa rapa Nay Wa Mitego ya kuitwa ‘Tumerogwa’. Kwenye ‘Tumerogwa’ Nay anashangaa namna ambavyo watanzania hawaridhiki na viongozi wanaowapata na kupitia mistari ya ngoma hii. Nay anatoa pongezi kwa baadhi ya viongozi waliopita kutoka Tanzania ikiwemo aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano John Pombe Magufuli.

https://www.youtube.com/watch?v=zNiO4t3n6Bs

Pepetua - Nedy Music

Kama wewe ni muumini wa kwenda klabu na sehemu tofauti tofauti za starehe, basi bila shaka unahitaji kutega sikio lako wimbo mpya kabisa wa Nedy Music wa kuitwa ‘Pepetua’. Huu ni wimbo ambao unazidi kuwaaminisha watanzania kuwa Nedy Music ni mtunzi bora na ana ujanja wa aina yake kwenye utunzi wa mashahiri bila kusahau video ya ngoma hii ambayo imeakisi mazingira ya klabu.

https://www.youtube.com/watch?v=KSsr84sh9T4

 Kafubaa - Mzee wa Bwax ft Zungu Macha

Huu ni wimbo ambao kwa sasa umesambaa sana kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Whatsap na Instagram hasa kutokana na mashahiri yake ambayo bila shaka yatamvutia na kumfurahisha yeyote atakayesikiliza. Kwenye singeli hii, Mzee wa Bwax anatoa maneno ya kashfa kwa mpenzi wake wa zamani ambaye anaonekana kudorora kimaisha huku akitumia mdundo uliotayarishwa na Eyoo Kenny kufikisha ujumbe wake huo.

https://www.youtube.com/watch?v=gSyp-kWmohg

Champino - Harmonize ft Fik Fameica

Ushirikiano mzuri kati ya wasanii hawa wawili ndio umepelekea ngoma hii kutoka kwa Harmonize wa Tanzania na Fik Fameika wa Uganda kuwa bora sana kiasi cha kufanya ngoma hii kutazamwa mara laki tatu ishirini na tatu ndani ya siku saba tu.

https://www.youtube.com/watch?v=sB6iUIs-ilk

Nitumie Link - Nikki Mbishi

Nikki Mbishi ametumia ubunifu wa aina yake kuja na wazo la ngoma hii ambayo rapa huyu anaanika kwa wasikilizaji utamaduni ulioshika kasi hivi sasa wa kusambaza mtandaoni picha na video zisizo na maadili almaarufu kama ‘connection’.

https://www.youtube.com/watch?v=6bFZCl7-TxI

Leave your comment