Hanscana, Lava Lava na Mbosso Wafichua Changamoto Wanazopitia Kufanya Video Kwenye Vivutio Vya Utalii
23 February 2022
[Picha: Ghafla]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Muongozaji video mashuhuri kutoka Tanzania Hanscana hivi karibuni ameeleza changamoto ambazo hupitia pindi anapotaka kufanya video kwenye vivutio mbalimbali vya utalii nchini Tanzania.
Hanscana ambaye ana wasifu wa kufanya kazi na wasanii mashuhuri nchini kama Diamond Platnumz, Ali Kiba na Harmonize kupitia akaunti yake ya Instagram alitanabaisha kuwa mamlaka zinazohusika kusimamia vivutio vya utalii aghalab hukatisha tamaa wasanii kufanya video kwenye vivutio hivyo.
Pakua Nyimbo za Alikiba Bila Malipo Kwenye Mdundo
Hanscana alitolea mfano video ya ‘Only You’ yake Mac Voice na Mbosso ambayo walipanga kuifanyia kwenye magofu ya huko Kilwa lakini uongozi wa eneo hilo walitaka kiasi kikubwa sana cha pesa hivyo wakaamua kufuta mpango huo wa kufanya video kwenye eneo hilo la kihistoria.
"Moja ya changamoto tunayopitia kwenye kushoot nchini ni tozo nyingi mno tunapohitaji kushoot kwenye vivutio vya utalii vya taifa (NATIONAL PARK) Wakati tukishoot hapo ni moja ya sehem kubwa ya kutangaza vivutio vyetu. Eg hii video tulishoot Kilwa Masoko ila tulivohitaji kushoot kwenye magofu ya kale uongozi wa pale walihitaji hela nyingi mmno tena kwa Dollar sio TSH na hawakutaka maongezi kabisa Mpaka tukaamuwa ku cancel. Shida sio kulipia shida ni unalipia kuitangaza nchi hapo ndo uzalendo unapokosa maana" aliandika Hanscana kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Soma Pia: Vitu Muhimu Wasanii wa Bongo Wanafaa Kujua Kabla ya Kujiunga na Lebo za Muziki
Waraka huo kutoka kwa Hanscana uliungwa mkono na Mbosso ambaye nae alilalamika kuwa ukiweka kando muda mrefu unaotumia kupata kibali cha kufanya video kwenye vivutio vya utalii, bei kubwa ambayo wasanii hutozwa na mamlaka husika ni kitu ambacho kinakatisha tamaa sana.
"Tatizo sio kulipia locations ila inaumiza sana unaenda kushoot mazingira ya nchi yako kuyatangaza na bado unapewa bei za tamaa.. Inarudisha sana nyuma," ulisomeka sehemu ya ujumbe huo kutoka Mbosso ambaye baadhi ya video zake kama zimefanyika kwenye vivutio vya utalii.
‘Nadekezwa’, ‘Ate’ na ‘Hodari’ zilifanyika maeneo ya vivutio vya utalii.
Mtunzi wa ngoma ya ‘Inatosha’ yaani Lavalava nae hakufanya ajizi kutoa ya moyoni kwa kuandika kuwa muda na gharama ya kupiga tu picha kwenye vivutio vya utalii bado ni changamoto sana.
"Nilishawahi Kutaka kupiga picha ya cover yawimbo wangu sehemu fulani nikaambiwa gharama yake ni milioni tano zakitanzania na niandike barua kwanza baada ya mwezi ndoijibiwe sasa sijui nikwanini alafu angetaka raia wa nchi nyingine angepewa hata kwabure yani bongo sijui wanamatatizo gani," aliandika Lavalava kwenye chapisho hilo la Hanscana.
Kufikia sasa, bado mamlaka zinazohusika na masuala ya utalii hazijasema chochote kuhusiana na madai hayo ambayo kwa muda sasa yamekuwa ni changamoto kwa wasanii.
Leave your comment