Diamond ‘Gidi’, Whozu ‘Ding Dong’ na Nyimbo Zingine Mpya Bongo Wiki Hii

 

Kiwanda cha muziki nchini Tanzania kimezidi kunoga huku wasanii wakiachia ngoma mpya ambazo zimeshika hisia za wapenda Bongo Fleva hapa nchini Tanzania. Zifuatazo ni ngoma tano mpya kutoka kwa wasanii wa Tanzania kwa wiki hii:

Pakua Nyimbo za Whozu Bila Malipo Kwenye Mdundo

Gidi - Diamond Platnumz

Mdundo mkali kutoka kwa S2kizzy ndio umemrudisha Diamond Platnumz kwenye masikio ya watanzania kupitia ngoma yake ya ‘Gidi’. Mdundo wa wimbo mpya , mirindimo na midondoko yake ni ushahidi tosha kuwa Diamond Platnumz ni fundi wa kutengeneza muziki wenye ubora.

https://www.youtube.com/watch?v=BRsoOKdmKic

Ding Dong - Whozu

Kama kuna mtoto wa mtu anakupenda, basi Whozu ameileta kwako ‘Ding Dong’ ngoma ambayo anakiri kwa uwazi kabisa jinsi huba kutoka kwa mpenzi wake limemkolea.

https://www.youtube.com/watch?v=yseqVJdawLM

Young Love - Fid Q & Oduma Esan

Baada ya ukimya wa miezi takriban sita, wiki hii Fid Q alichangamsha watanzania na ‘Young Love’. Ngoma hii imeonesha upande wa pili wa Fid Q na ufundi wake kwenye kutunga mashairi ya mapenzi ambayo yataburudisha wasikilizaji.

https://www.youtube.com/watch?v=r8sd2grKI4M

Soma Pia: Rekodi 5 Diamond Platnumz Ameweka Kwenye Muziki wa Bongo Fleva

Chipsi - Motra The Future ft G Nako

Moto wa Motra The Future kwenye muziki bado unawaka na ngoma yake mpya ya kuitwa ‘Chipsi’. Ndani ya  ‘Chipsi’, Motra ametupa vijembe vya aina yake kwa watu wasiomtakia mema kwenye muziki wake. G Nako ambaye ni mojawapo ya wasanii wanaounda kundi la Weusi amesikika kwenye ngoma hii hasa upande wa kiitikio.

https://www.youtube.com/watch?v=OOzoIl0ocQo

Mama - Chege ft Christian Bella

Maneke pamoja Mocco Genius ndio wamehusika kuandaa ngoma hii ya ‘Mama’ ambayo inamkutanisha Chege na Christian Bella. Ingawa ni mara ya kwanza kwa miamba hawa kufanya kazi pamoja, Chege na Bella wametoa kazi nzuri. Muingiliano mzuri wa sauti na mashahiri mujarab ni moja kati ya vitu vinavyofanya ngoma hii kuwa ya kipekee mno.

https://www.youtube.com/watch?v=gVGkifrAYqg

Wasanii wengine ambao wametoa ngoma wiki hii ni pamoja na Baba Levo ‘Hellow’, Dizasta Vina ‘Confession of a Madman’ pamoja na Frida Amani ‘Fala Mimi’.

Leave your comment