Rekodi 5 Diamond Platnumz Ameweka Kwenye Muziki wa Bongo Fleva

[Picha: The Citizen]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Diamond Platnumz amekua mojawapo ya mada kubwa kwenye mitandao ya jamii Tanzania baada ya kuchapisha ujumbe kuhusu muziki wa Bongo kwenye instastory yake. Kwenye ujumbe huo, Diamond Platnumz alionesha kiu yake ya kutaka kuona muziki wa Bongo Fleva unafika mbali.

Pakua Nyimbo za Jux Bila Malipo Kwenye Mdundo

Diamond alisema anatamani kuona wasanii wa Tanzania wanashindana na wasanii wa kimataifa. Ndoto hii ya Diamond Platnumz huenda ikatimia kwani yeye ni msanii ambaye tangu aanze muziki mwaka 2009 hajawahi kurudi nyuma.

Soma Pia: Nandy, Jux, Mbosso na Wasanii Wengine Bongo Wanaotajarajiwa Kuachia Video Mpya

Diamond Platnumz ameweka rekodi kadhaa nchini Tanzania na kimataifa. Kwenye nakala hii, tunaangazia rekodi tano ambazo Diamond Platnumz ameweka kwenye muziki wa Tanzania:

Tuzo

Tangu kuanza kwa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ndiye msanii anayeongoza kuwa na tuzo nyingi zaidi, tayari akiwa na tuzo zaidi ya 65. Mei 3 mwaka 2014, kwenye tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) Diamond Platnumz aliweka rekodi ya kupata tuzo 7 ndani ya usiku mmoja. Kando na KTMA, Diamond ana tuzo zingine za kimataifa kama vile, Afrimma, Chanel O, AEUSA na Soundcity kama msanii bora wa kiume mwaka 2018.

Pakua Nyimbo za Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

YouTube

Ukiachilia mbali rekodi yake ya kuwa msanii wa kwanza nchini Tanzania na kusini mwa Jangwa la Sahara kufikisha watazamaji Bilioni moja kwenye akaunti yake ya YouTube, pia tusisahau kuwa wafuasi wake Milioni 6 Youtube wamemfanya Diamond Platnumz kuwa msanii anayeongoza kuwa na wafuatiliaji wengi zaidi Tanzania kwenye mtandao huo. Aidha, video yake ya ‘Yope Remix’ ndio video inayoongoza kutazamwa zaidi YouTube tangu kuumbwa kwa Tanzania, ikifuatiwa na ‘Inama’ pamoja na ‘Waah’ ambayo amefanya na Koffi Olomide.

Mitandao ya kijamii

Diamond Platnumz anaongoza kuwa na wafuasi wengi zaidi kuliko msanii au mtu yeyote yule nchini Tanzania. Ukijumlisha wafuasi wake wa mitandao mitatu mikubwa, Diamond ana wafuasi takriban Milioni 21 kwa ujumla. Diamond ana wafuasi Milioni 14 Instagram , Milioni 6 Facebook pamona na Milioni 1 huko Twitter.

Collabo za Kimataifa

Ngoma ya ‘My Number One Remix’ ya mwaka 2014 akiwa na Davido ndio ilimfanya Diamond Platnumz awe  nyota wa muziki barani Afrika. Kutokea hapo, ameshafanya collabo na wasanii kama Mr Flavour, Iyanya, P Square, Tiwa Savage na wengineo kutoka Nigeria. Kutokea nchini Marekani Diamond ameshafanya kazi na wasanii kama Rick Ross, Alicia Keys na Marion aliyemshirikisha kwenye ‘African Beauty’.

Matamasha

Diamond Platnumz ametumbuiza kwenye majukwaa makubwa ambayo bado wasanii wengi watanzania hawajafika. Mwaka 2016, Diamond Platnumz alitumbuiza kwenye jukwaa la MTV Mama huko Afrika Kusini. Pia ameshashiriki kwenye tamasha la One Africa Music Fest zaidi ya mara moja akiwa na magwiji wa Afrika kama Davido, Tiwa Savage, Stonebwoy, Sarkodie, Mr Flavour na wengineo wengi. Kubwa kabisa ni yeye kushiriki kutumbuiza kwenye tamasha linaondaliwa na Recording Academy ambayo ni kamati ya waandaji wa tuzo za Grammy siku chache zilizopita, kitu ambacho kilikuwa hakijawahi kutokea kwenye historia ya Tanzania.

Leave your comment