Nandy, Jux, Mbosso na Wasanii Wengine Bongo Wanaotajarajiwa Kuachia Video Mpya

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Siku za hivi karibuni, kumeibuka mtindo wa wasanii wa Tanzania kupendelea kuachia audio ya wimbo kwanza na kisha baadaye kuachia video ambayo huongeza ladha. Zifuatazo ni video tano kutoka kwa wasanii watanzania ambazo mashabiki wanazisubiri kwa hamu:

Kunjani - Nandy

Januari 12 mwaka huu, Nandy kupitia akaunti yake ya Instagram alidokeza kuwa video ya ‘Kunjani’ ft Sho Madjozi iko tayari. "Hamjambo ndo tuko tayari kuwapa video," aliandika Nandy kwenye akaunti yake ya Instagram. ‘Kunjani’ inatarajiwa kuwa video ya pili kutoka kwa Nandy mwaka huu. Mapema mwaka huu, Nandy aliachia video yake ya ‘Party’ ambayo alifanya na Billnass pamoja na Mr Eazi kutoka Nigeria.

Pakua Nyimbo za Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

https://www.youtube.com/watch?v=33QNth6LAhM

I Love You - Jux

Kwenye ‘I Love You’, Jux  amemshirikisha msanii kutokea Ghana Gyakie. Pamoja na kwamba Jux bado hajatangaza kuachia video ya ngoma hiyo, mshabiki wengi wameonekana kuwa na hamu ya video hiyo. ‘I Love You’ ni ngoma ya pili Jux kufanya na msanii wa Afrika Magharibi. Ngoma ya kwanza Jux kufanya na msanii wa Afrika Magharibi inaitwa ‘Fashion Killer’ akiwa na Singah kutokea Nigeria ngoma ambayo Jux aliiachia mwaka 2020.

Pakua Nyimbo za Jux Bila Malipo Kwenye Mdundo

https://www.youtube.com/watch?v=Q_NxJF8nM14

Te Quiero - Rayvanny ft Marioo

Rayvanny ana deni kubwa sana kwa mashabiki zake kwani baada ya kuwaonjesha utamu wa ngoma ya ‘Te Quiero’, kazi iliyobaki ni kukata kiu kabisa kwa kuachia video. Ndani ya muda mfupi, ‘Te Quiero’ imeweza kupata mafanikio makubwa kwani ndani ya siku saba tu, kupitia mtandao wa YouTube tayari audio ya ngoma imeshatazamwa takriban na watu laki tatu ishirini na moja elfu. Video ya ‘Te Quiero’ inatarajiwa kuwa videi ya tatu kutoka kwa Rayvanny baada ya kuachia ‘Rara’ pamoja na ‘Stay’ ambayo alimshirikisha Abby Chams.

Pakua Nyimbo za Marioo Bila Malipo Kwenye Mdundo

https://www.youtube.com/watch?v=2UPOR5lbzeY

Tausi - Mrisho Mpoto & Mbosso

Hakuna shabiki wa muziki mzuri asiye na hamu ya kupata kuona video ‘Tausi’ kutoka kwa Mrisho Mpoto na Mbosso. Kufikia sasa, Mbosso ameshashiriki video za muziki zaidi ya 50 lakini video ya ‘Tausi’ inatarajiwa kuwa ya kipekee kwani wote tunajua ubunifu na utofauti ambao Mrisho Mpoto hutumia kwenye video ambazo huwa anashiriki.

https://www.youtube.com/watch?v=GKtz_kLRWVA

Pain Killer - Kusah ft Kataleya & Kandle

Ngoma hii ni ya kwanza kwa Kusah kufanya na wasanii kutoka Uganda hivyo mengi zaidi yanatarajiwa kutoka kwenye video hii. Aidha, kwa muda sasa, Kusah amekuwa akifanya video na waongoza video kutoka Tanzania hivyo wengi wana hamu ya kufahamu ni director gani ambaye atafanya kazi na Kusah kwenye ngoma hii.

Pakua Nyimbo za Kusah Bila Malipo Kwenye Mdundo

https://www.youtube.com/watch?v=l5dnj8_wP3g

Leave your comment

Top stories

More News