Valentines 2022: Nyimbo Bora za Kusikiliza Siku ya Wapendanao

[Picha: Sharon Madonna]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kuna namna nyingi sana ambazo unaweza kumtakia heri mpenzi wako hasa itakapofika Februari 14. Unaweza ukatuma maua, ukapeleka kadi kwa mpenzi wako au njia rahisi unaweza ukatuma ngoma kali ya mapenzi ili uweze kumwambia kwa urahisi unajisikiaje juu yake. Kwa kulitambua hilo tumeamua kukuletea ngoma 10 kali ambazo unaweza kuzisikiliza kipindi cha Valentine:

Pakua Nyimbo Zake ALi Kiba Bila Malipo Kwenye Mdundo

Valentine - Rayvanny

Pamoja na kwamba wimbo huu alimuimbia mpenzi wake Paula, lakini bila shaka wimbo huu ni makhususi kwa ajili ya kuonesha mapenzi uliyonayo kwa msichana wako.

https://www.youtube.com/watch?v=TWbPaDHonrc

For You - Marioo

Kama una mpenzi ambaye anakusaidia, kukupa moyo na ambaye alitibu majeraha yako ya moyo kutokana na kuumizwa basi ‘For You’ ni wimbo ambao unamfaa sana hasa kipindi hiki cha Valentine.

https://www.youtube.com/watch?v=e3Aym00lfB4

Pakua Nyimbo za Marioo Bila Mlaipo Kwenye Mdundo

Never Ever - Vanessa Mdee

Kwenye ngoma hii ya RnB Vanessa anaapa kuwa na mpenzi wake milele yote na kamwe hatakuja kumuacha kutokana na penzi lake kuwa la moto sana.

https://www.youtube.com/watch?v=si4YNX4O5f4

Tamba - Mbosso

Kwenye kibao hiki, Mbosso anawakumbusha watu kuwa mapenzi ya dhati hayahitaji kuwa na pesa nyingi sana. Kikubwa ni watu wapendane na kukubaliana bila tashwishwi.

https://www.youtube.com/watch?v=tg5hw8K6UoQ

Valentine - Genius Jini ft Jay Melody

Kama una mpango wa kumpeleka mpenzi wako ‘Out’ siku ya Valentine, ni vyema ukakubali kusindikizwa na wimbo huu ambao ukiweka kando mashahiri yake, pia mdundo wake unaruhusu wapendanao kucheza pamoja.

https://www.youtube.com/watch?v=Xcw8TNHH7R4

Utu - Ali Kiba

Kama unatafuta chaka la mapenzi na kumkumbusha mpenzi wako sifa zake na jinsi anavyokufanya ujisikie vizuri, basi ‘Utu’ ya Alikiba ni kwa ajili yako.

https://www.youtube.com/watch?v=PkXxm2tCtgs

Raha - Zuchu

Kwenye ngoma hii Zuchu anakiri kabisa kuwa anajisikia vizuri sana kupendwa kutokana mapenzi moto moto anayopewa na mpenzi wake.

https://www.youtube.com/watch?v=oLlJcWqmb_U

Kiboko Yangu - Mwana FA ft Ali Kiba

Ni binadamu gani ambaye anakufahamu nje ndani na unahisi ni kiboko? Kama ni mpenzi wako basi bila shaka hii ni ngoma makhususi kwa ajili ya kumtumia mtu ambaye utashiriki nae Valentine hii.

https://www.youtube.com/watch?v=mAcuWgX_X10

Komela - Dayna Nyange ft Billnass

Ukitaka kumhakikishia mpenzi wako kuwa unampenda hasa kipindi hiki cha Valentine basi huna budi kusikiliza ‘Komela’ ya Dayna Nyange, ngoma ambayo ndani yake imejaa mashairi mazuri ya mapenzi.

https://www.youtube.com/watch?v=tMnt3tbSJEE

My Number One - Diamond Platnumz

Ukitaka kumwaminisha mwandani wako kuwa yuko peke yake na kwamba unaye yeye peke yake, basi Diamond Platnumz amekusaidia kufikisha ujumbe huo kupitia ‘My Number One’.

https://www.youtube.com/watch?v=64riif8FfNI

Leave your comment