Nyimbo Mpya: Kusah Aachia Ngoma Mpya ‘X’

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Kusah ameachia ngoma mpya ya kuitwa ‘X’.

‘X’ ni wimbo wa mapenzi ambao ndani yake Kusah anamuelezea kwa kina mpenzi wake wa sasa, jinsi ambavyo mpenzi wake wa zamani yaani ‘X’ anavyomfuatilia na kuweka vikwazo kwenye penzi lao.

Pakua Nyimbo Zake Kusah Bila Mlaipo Kwenye Mdundo

"Mwenzako X kutwa haishi kuntaja. Kifupi maex wanateseka na haja tumewapiga X si walitaka shindana. Si walitaka pira wale tumewatoa bila si walitaka kuzira basi wamepoteza dira," anaimba Kusah kwenye aya ya kwanza.

Maudhui ya ngoma hii huenda yakashabihiana na ngoma ya ‘Ex Wangu Remix’ ya Hamisa Mobeto na Seneta Kilaka, ila kinachonogesha zaidi ngoma hii ni utunzi mzuri wa mashahiri kutoka Kusah pamoja.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Zilizoachiwa Bongo Wikendi Iliyopita [Video]

Ngoma hii imetayarishwa na Bonga mtayarishaji wa muziki kutoka Tanzania ambaye kwa muda sasa alikuwa akifanya kazi na Harmonize. Pia ameshiriki kuaandaa ngoma ya kuitwa ‘Mama’ ya kwake Nay Wa Mitego.

‘X’ ni ngoma ya tatu kutoka kwa Kusah kwa mwaka huu wa 2021, ngoma nyingine kutoka kwa msanii huyo kwa mwaka huu ni pamoja na ‘I Don't Care’ pamoja na ‘Pain Killer’ ambayo ameshirikiana na kundi la muziki kutoka nchini Uganda Kataleya na Kandle.

https://youtu.be/5cDFuIPkFrY

Leave your comment