Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Zilizoachiwa Bongo Wikendi Iliyopita [Video]

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wasanii wa Tanzania wanaendelea kuachia kazi mpya zinazopokelewa vizuri. Katika nakala hii tunaangazia nyimbo tano zilizoachiwa ndani ya wikendi iliyopita.

Rostam ft Ferooz - Hujambo Mwanangu

Kwenye wimbo huu, Rostam wamemshirikisha msanii mwenzao maarufu Ferooz. Katika mistari yao, wanaangazia kazi mpya ya Rais Samia. Kufikia sasa wimbo huu una watazamaji zaidi ya laki moja kwenye YouTube. Kanda yake inatarajiwa hivi karibuni.

https://www.youtube.com/watch?v=Ql4wkqmqyQ8

Do Lemme - Go MC Kinata ft Ibraah

Huu ni wimbo wa Singeli wake MC Kinata ambao alimshikisha Ibrah kutoka Konde Music Worldwide. Kwenye mistari yao Kinata, anaimba kuhusu upendo huku Ibraah akitupa michambo. Kufikia sasa ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya laki nne kwenye YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=uPU4Tjh1qSk&ab_channel=IbraahIbraah

Kudimbwi - Meja Kunta

Huu ni mdundo mpya wa Singeli kutoka kwa Meja Kunta. Anaimba kuhusu mada tofauti tofauti katika wimbo huu. Kufikia sasa ni wimbo unaoendelea kupata umarufu na watazamaji zaidi ya elfu thelathini na nne kwenye YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=M_5yV0znuFU&ab_channel=MejaKuntaMejaKunta

Nilewe - Kusah Ft Linah

Gwiji wa nyimbo za mapenzi Kusah amemshirikisha Linah kuangazia jinsi alivyoumizwa kwenye uhusiano. Kufikia sasa, wimbo huu umefikisha watazamaji zaidi ya elfu thelathini na tano kwenye YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=ctKYJFIDty4&ab_channel=Kusah

Press Conference - Nacha

Msanii Chipukizi wa Hip-hop Nacha ameachia wimbo huu mpya kuangazia mada kadha ikiwemo namna waandishi wa habari wamechagua wasanii bora hivyo kuwadhalilisha wanaochipuka.

https://www.youtube.com/watch?v=0CC-Z42xsI0&ab_channel=NachaMusicNachaMusic

Leave your comment