Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia ‘Flowers II’ EP

[Picha: The City Celeb]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Rayvanny ameachia EP yake mpya aliyoipa jina la ‘Flowers II’ EP.

‘Flowers II’ imeundwa na maudhui ya mapenzi kuanzia kwenye ngoma ya kwanza mpaka ya mwisho. Hii ni muendelezo wa Rayvanny kuachia EP msimu wa Valentine kama alivyofanya mwezi Februari mwaka 2020 alipoachia ‘Flowers’ EP.

Pakua Nyimbo za Nadia Mukami Bila Malipo Kwenye Mdundo

‘Flowers II’ ni EP iliyosheheni ngoma 8 na ngoma 3 ambazo ni ‘I Miss You’ ft Zuchu ‘Wanaweweseka’ na ‘Sweet’ ft Guchi tayari zilikuwa zimeshatoka hivyo kufanya ngoma tano zilizobaki kuwa mpya kabisa.

Wasanii wengine walioshirikishwa kwenye EP hii ni pamoja na Nadia Mukami kwenye ‘Falling in Love’, Marioo kwenye ‘Te Quiero’, Roki kutokea Zimbabwe kwenye ‘My Love’ pamoja na mkongwe wa muziki kutoka Tanzania Ray C ambaye ameshiriki kwenye ngoma ya ‘Honey’.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: RJ the DJ Aachia ‘Sitamani’ Akiwashirikisha Loddy Music na Young Lunya

‘Te Quiero’ akiwa na Marioo ni mojawapo ya ngoma ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu sana kutoka kwenye EP Hii.  Rayvanny na Marioo wameweza kukata kiu ya mashabiki zao kwani ukiweka kando muingiliano na mpangilio mzuri wa sauti, pia uandishi na utunzi wa ngoma hio umeweza kufana sana.

EP ya ‘Flowers II’ imeandaliwa na watayarishaji wa muziki nguli kutoka Tanzania yaani Sound Bwoy pamoja na Lizer Classic huku maandalizi ya mwisho yakishughulikiwa na Nusder pamoja na Motif kutokea nchini Kenya.

Soma Pia: Harmonize Atangaza Wasanii Watakaotumbuiza Kwenye Tamasha Yake ya Afro East Carnival

Ikumbukwe hii ni EP ya tatu kutoka kwa Rayvanny tangu aanze muziki, EP nyingine ni pamoja na ‘Flowers’ ya mwaka 2020 pamoja na ‘New Chui’ ya mwaka 2021.

Leave your comment