Nyimbo Mpya: RJ the DJ Aachia ‘Sitamani’ Akiwashirikisha Loddy Music na Young Lunya

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

DJ rasmi wa Diamond Platnumz RJ the DJ ameachia ngoma mpya aliyoipa jina la ‘Sitamani’ ambayo amewapa shavu wasanii wawili; Loddy Music pamoja na rapa Young Lunya.

Hii ni ngoma ya kwanza kutoka kwa RJ the DJ kwa mwaka huu wa 2022 na imetimia takriban miezi mitatu tangu aachie kibao chake cha ‘Hennesy’.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Dully Sykes Aachia Ngoma Mpya ‘Unanipagawisha’

Ngoma hii inafunguliwa kwa sauti nzuri ya Loddy Music ambaye anaonesha ni kwa namna gani anampenda mpenzi wake, huku akihadithia wasikilizaji jinsi mrembo wake huyo alivyokuwa mzuri.

"Yani una adabu yo kind nahisi nikimcheat namuonea. She call me lover lover mchumba kanifollow. Na tabasamu lake linanimaliza. Moyo unaruka ruka mtoto unanikimbiza. Ananimurder usiku kwenye giza. Hizo style za kufakufa zote tushazimaliza," anaimba Loddy Music kwenye aya ya kwanza.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Jux ‘I Love You’, Maua Sama ‘Shukurani’ na Nyimbo Zingine Mpya Zilizoachiwa Wiki Hii

Rapa Young Lunya anasikika zaidi kwenye aya ya pili ya ngoma hii ambapo nae anamwaga sifa nyingi sana kwa mpenzi wake.

Ngoma hii ni muendelezo wa RJ The DJ kupendelea kufanya kazi na Young kwani wawili hao walishawahi kufanya ngoma ya pamoja ya kuitwa ‘Muonjeshe’ ambayo Young Lunya alifanya na Mimi Mars pamoja na G Nako.

https://youtu.be/LX2CLMjCduk

Leave your comment