Nyimbo Mpya: Jux ‘I Love You’, Maua Sama ‘Shukurani’ na Nyimbo Zingine Mpya Zilizoachiwa Wiki Hii

[Picha: Citi Muzik]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Imekuwa ni wiki yenye pilika pilika nyingi sana kwenye uwanja wa muziki nchini Tanzania kwani wasanii mbalimbali wametoa nyimbo na miradi ya muziki kwa lengo la kukosha hisia za mashabiki zao. Zifuatazo ni nyimbo tano kali kutoka kwa wasanii wa Tanzania kwa wiki hii :

Soma Pia: Video ya ‘Waah’ ya Diamond Platnumz Yafikisha Watazamaji Milioni 100

I Love You - Jux ft Gyakie

Mashahiri ya ngoma hiii yanaendana kabisa na wakati uliopo kuelekea msimu wa Valentine. Bila shaka Jux amezidi kuonesha umahiri wake kwenye RnB kupitia ngoma hii na Gyakie kutokea Ghana, ngoma ambayo kufikia sasa imeshatazamwa mara tisini na tano elfu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=Q_NxJF8nM14

Pakua Nyimbo za Jux Bila Malipo Kwenye Mdundo

Shukurani - Maua Sama

Ukiweka kando sauti nzuri ya Maua Sama, kitu kingine kinachovutia kwenye ‘Shukurani’ ni ujumbe wake ambao Maua Sama anashukuru kwa Mwenyezi Mungu kwa kuweza kufika hapo alipofika leo. Kama unatafuta wimbo ambao utakupa hamasa, faraja na tumaini la kuendelea mbele basi ‘Shukurani’ kutoka kwa Sama ni kwa ajili yako.

https://www.youtube.com/watch?v=5SUefw-MUls

Pakua Nyimbo za Maua Sama Bila Mlaipo Kwenye Mdundo

Saraphina – Wamerudiana

Kwenye ngoma hii ambayo imetayarishwa na Aloney M, Saraphina anaimba kwa hisia sana akilalamika namna ambavyo mpenzi wake amemuacha na kumrudia mpenzi wake wa zamani.

https://www.youtube.com/watch?v=_iYZphrap7U

Pain Killer - Kusah ft Kataleya & Kandle

Kusah ameendelea kuthibitisha ubora wake kwenye utunzi wa ‘Pain Killer’, ngoma ambayo ukiweka kando ujumbe wake uliobeba hisia kali za mapenzi pia ushirikiano wa kushiba uliooneshwa kati ya Kusah na kundi la Kataleya & Kandle kutoka Uganda.

https://www.youtube.com/watch?v=l5dnj8_wP3g

Ivo Ivo - Baddest 47

Mfalme wa Street Vibes, Baddest 47 amerudi tena na ngoma yake ya ‘Ivo Ivo’ ambayo inatarajiwa kurindima kwenye spika za klabu na sehemu mbalimbali za starehe hapa nchini Tanzania. Wimbo huu umeundwa na mdundo wenye nguvu pamoja na mashairi shirikishi ambayo bila shaka yatamfanya mtu yeyote kuamka na kuanza kucheza.

https://www.youtube.com/watch?v=aT6XBi0S0Ug

Leave your comment