Video ya ‘Waah’ ya Diamond Platnumz Yafikisha Watazamaji Milioni 100

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutoka nchini Tanzania Diamond Platnumz amezidi kuweka historia kwenye muziki wa Bongo Fleva baada ya video yake ya "Waah" kuweza kutazamwa mara Milioni 100 kwenye mtandao wa YouTube.

Video ya ‘Waah’ iliachiwa Novemba 30 mwaka 2020 na hivyo video hii imechukua miezi 14 tu kuweza kufikisha watazamaji Milioni 10.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu Aachia Video ya ‘Mwambieni’  

Video hio haijavunja rekodi ya ngoma ya ‘Yope Remix’ ambayo ilifikisha watazamaji Milioni 100 ndani ya miezi 10 pekee.

Video ya ‘Waah’ inakuwa ni video ya tatu kutoka kwa Diamond Platnumz kufikisha watazamaji Milioni 100 kwani video nyingine ni pamoja na ‘Yope Remix’ ambayo kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 178 pamoja na ‘Inama’ ambayo kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 104 kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Diamond, Harmonize na Wasanii Wengine Waliotazamwa Zaidi YouTube Tanzania Januari 2022

Aidha, kutoka kwenye video ya ‘Waah’, Diamond Platnumz aliweza kuweka rekodi tofauti tofauti ikiwemo ‘Waah’ kutazamwa mara laki moja ndani ya saa moja, rekodi ambayo Harmonize alikuja kuivunja kupitia video yake ya ‘Attitude’ ambayo ilitazamwa mara laki moja ndani ya dakika 44 tu.

Pia, ‘Waah’ iliweza kuweka rekodi mpya kwenye muziki wa Afrika baada ya kufikisha watazamaji Milioni 1 ndani ya saa 8 tu na hivyo kupiku rekodi ya Davido ambaye video yake ya ‘Fem’ ilitazamwa mara Milioni 1 ndani ya saa 9.

Ikumbukwe pia kuwa Diamond Platnumz ndie msanii anayeongoza kuwa na wafuatiliaji wengi zaidi kusini mwa jangwa la sahara akiwa na wafuatiliaji Milioni 6 kwenye akaunti yake hiyo huku akiwa ameshatazamwa mara Bilioni 1.6 kwenye mtandao wa YouTube.

Leave your comment

Top stories

More News