Diamond, Harmonize na Wasanii Wengine Waliotazamwa Zaidi YouTube Tanzania Januari 2022

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

 YouTube ni mojawapo ya mitandao ambayo wasanii hupendelea kuweka kazi zao za muziki. Kwa mwezi Januari 2022, mambo yamezidi kuwa sukari kwenye mtandao huo kwani kuna baadhi ya wasanii wameweza kufanya vizuri kwa kutazamwa zaidi.

Wafuatao ni wasanii watano ambao wametazamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube kwa mwezi Januari mwaka 2022:

Soma Pia: Diamond, Rayvanny Watajwa Miongoni Mwa Wasanii Wa Afrika Waliotazamwa Zaidi YouTube 2021

Diamond Platnumz

Ufalme wa Diamond Platnumz kwenye mtandao wa YouTube bado unaendelea kwani kwa mwezi Januari ametazamwa mara Milioni 32.2. Yeye ndiye msanii aliyeongoza kutazamwa zaidi mwezi Januari kwenye mtandao wa YouTube.

Rayvanny

Bila shaka ngoma yake ya ‘Rara’, video ya ‘Stay’ pamoja na ngoma ya ‘I Miss You’ aliyomshirikisha Zuchu ndio zimechagiza Rayvanny kutazamwa takriban mara Milioni 18.7 kwenye YouTube.

Soma Pia: Nandy Atangaza Ujio wa Colabo Zake na Davido, Patoranking, Sauti Sol na Dulla Makabila

Harmonize

Mwaka 2022 umezidi kunoga kwa Teacher Konde kwani kwa mwezi Januari pekee ametazamwa takriban mara Milioni 16 kwenye mtandao wa YouTube. Yeye ndiye msanii pekee kutokea Konde Gang kuingia kwenye orodha hiii.

Mbosso

Licha ya kwamba ameachia ngoma moja tu ya ‘Tausi’ kwa mwezi Januari, Mbosso ametazamwa mara Milioni 10.2 kwenye mtandao huo wa YouTube. Yeye ndiye msanii wa nne kutazamwa zaidi YouTube kwa mwezi Januari.

Zuchu

Kwa mwezi Januari, Zuchu ameweza kutazamwa takriban Milioni 9.9 kwenye mtandao wa YouTube. Kwa mwezi huo, Zuchu alitoa ngoma moja pekee ya kuitwa ‘Mwambieni’.

Leave your comment

Top stories

More News