Nandy Atangaza Ujio wa Colabo Zake na Davido, Patoranking, Sauti Sol na Dulla Makabila

[Picha: Trendy Beatz]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Nandy hivi karibuni amedokeza ujio wa collabo ambazo tayari ameshazikamilisha na anatarajia kuziachia kwa mashabiki zake hivi karibuni.

Mtunzi huyo wa ngoma ya ‘Nimekuzoea’ kupitia akaunti yake ya Instagram alitoa taarifa kwa mashabiki wake kuwa kufikia sasa ameshafanya collabo na wasanii kama Patoranking na Davido kutokea Nigeria, Sauti Sol kutokea Kenya pamoja na Dulla Makabila kutokea nchini Tanzania.

Soma Pia: Diamond, Rayvanny Watajwa Miongoni Mwa Wasanii Wa Afrika Waliotazamwa Zaidi YouTube 2021

Kupitia chapisho hilo aliwaomba mashabiki wampe chaguo ni ngoma gani aanze kuipeleka sokoni.

"Tuanze na collabo ipi : Nandy ft Patoranking, Nandy ft Davido, Nandy ft Sauti Sol, Nandy ft Dullah Makabila," aliandika Nandy.

Kando na Nandy, wasanii wengine wa Bongo ambao wameshafanya collabo na Davido ni pamoja na Diamond Platnumz kwenye ‘Number One Remix’, Joh Makini kwenye ‘Kata Leta’ pamoja na Dayna Nyange kwenye ‘Elo’.

Soma Pia: Rayvanny Atangaza Ujio wa EP ya ‘Flowers II’

Aidha kwa upande wa Sauti Sol, collabo hii inatarajiwa kuwa ya pili baina ya Nandy na bendi hio baada ya ngoma yao ya ‘Kiza Kinene’ ya mwaka 2019 kuweza kufanya vizuri sana hapa Afrika Mashariki.

Mashabiki pia wameonekana kuwa na shauku ya kuona collabo kati ya Nandy na Patoranking, msanii ambaye kufikia sasa ameshafanya kazi na wasanii wa Tanzania kama vile Navy Kenzo, Diamond Platnumz, Rayvanny pamoja na Ali Kiba.

Leave your comment