Rayvanny Atangaza Ujio wa EP ya ‘Flowers II’

[Picha: Rayvanny Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bosi wa lebo ya Next Level Music Rayvanny ametangaza ujio wa EP iliyopewa jina la ‘Flowers II’.

 Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny alitoa orodha ya nyimbo zilizomo kwenye EP hiyo. EP hiyo iko na jumla ya nyimbo tisa ambazo zimewahusisha wasanii kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Soma Pia: Diamond, Rayvanny Watajwa Miongoni Mwa Wasanii Wa Afrika Waliotazamwa Zaidi YouTube 2021

Wasanii walioshirikishwa kwenye EP hiyo ni pamoja na Zuchu, Roki, Nadia Mukami, Clyde, Guchi, Ray C na Marioo.

‘Flowers II’ inatarajiwa kutikisa tasnia ya muziki ya Tanzania kutokana na wasanii walioshirikishwa katika utengenezaji wake. Takriban wasanii wote mle ndani ni wenye heshima na mafanikio makubwa.

Soma Pia: Mac Voice Adokeza Kuachia Albamu

Kwa mujibu wa chapisho aliloliweka mtandaoni, EP hiyo itatoka rasmi mnamo tarehe 10 mwezi huu wa Februari.

Tayari ngoma ya kwanza kwenye EP hiyo ishatoka nayo ni ya ‘I Miss You’ ambayo ni kolabo aliyomshirikisha Zuchu. Ngoma hiyo iliyotoka tarehe 15 mwezi wa Januari imepata mapokezi mazuri.

Ndani ya takriban wiki mbili tu, ‘I Miss You’ ishasikizwa zaidi ya mara milioni moja kwenye mtandao wa YouTube, japo video rasmi bado haijatoka.

Ngoma hiyo imesukwa na mtayarishaji wa muziki Lizer Classic kutoka lebo ya WCB. Mwaka jana Rayvanny aliachia EP iliyopewa jina la ‘Flowers’, na EP hii inayotarajiwa kutoka ni muendelezo wa EP hiyo ya kwanza. Kwa sasa mashabiki wanasubiri kwa hamu sana EP ya ‘Flowers II’.

Leave your comment