Mac Voice Adokeza Kuachia Albamu

[Picha: IPP]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Mac Voice ameendelea kutoa habari njema kwa mashabiki zake baada ya kutangaza kuwa yuko kwenye mchakato wa kuachia albamu yake ya kwanza ya muziki.

Mac Voice ambaye ni msanii wa kwanza kutambulishwa chini ya lebo ya Next Level Music alitoa taarifa hizo kupitia chapisho lake la Instagram. Kwenye chapisho hilo, Mac Voice aliandika ujumbe mfupi ambao uliashiria kuwa anataka kuleta albamu mpya sokoni.

Soma Pia: Wasifu wa Mac Voice,maisha yake ya mapema, kazi yake ya sanaa...

"Album is loading" akimaanisha kuwa albamu iko mbioni kuachiwa. Kutoka kwa Mac Voice, albamu hiyo inatarajiwa kuwa ya kwanza kutoka kwake tangu ajiunge lebo ya Next Level Music, kwani kufikia sasa msanii huyo ameachia EP moja tu ya kuitwa ‘My Voice’.

EP hio ilimkaribisha vyema kabisa kwenye muziki wa Bongo Fleva kiasi cha kupata uteuzi kuwania kipengele cha msanii bora chipukizi barani Afrika kwenye tuzo za AEUSA.

Soma Pia: Wasanii Kutoka Tanzania Wanaotazamwa Zaidi Kwa Mwaka 2022

Hivyo basi, Mac Voice anaingia kwenye orodha ya wasanii ambao wanatarajiwa kuachia albamu hivi karibuni wengine wakiwa ni pamoja Ibraah, Marioo, Rosa Ree, Alikiba na wasanii wengine wengi.

Kwa sasa, macho na masikio ya mashabiki yameelekezwa kwenye himaya ya Next Level Music ili kufahamu tarehe, nyimbo pamoja na wasanii ambao watashiriki kwenye albamu hio.

Leave your comment