Wasifu wa Mac Voice,maisha yake ya mapema, kazi yake ya sanaa...
26 October 2021
[Picha: Mac Voice Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Mac Voice ni nani na ana miaka mingapi?
Jina la kisanii : Mac Voice
Jina halisi : Khamis Shaban Makalanga
Umri : Miaka 23
Aina ya muziki : Bongo Fleva
Thamani Ya Jumla : Haijulikani
Lebo : Next Level Music
Maisha ya Mapema ya Mac Voice yalikuwaje?
Mac Voice amezaliwa na kulelewa huko Bagamoyo mkoani Pwani na mama yake Mac Voice alikuwa anafanya biashara ndogo ndogo huku baba yake alikuwa anafanya kazi ya ualimu na wazazi wa Mac Voice walitengana kipindi akiwa na takriban miaka miwili hivyo kupelekea Mac Voice kuishi sana na mama yake.
Mac Voice alimaliza darasa la saba mwaka 2015 na aliishia kidato cha kwanza na aliamua kuacha shule kwa sababu mama yake alikosa pesa ya kumsomesha zaidi na kipindi bado anaishi Bagamoyo alishafanya kazi kwenye kiwanda cha wachina ambapo alihusika kukata miwa kwenye shamba, malipo yakiwa elfu hamsini kwa wiki na alifanya kazi hiyo kwa miezi sita.
Rayvanny Ashukuru Mashabiki Kwa Mapokezi Mazuri Waliompa Mac Voice
Mac Voice alianzaje muziki?
Mara baada ya kuacha shule Mac Voice aliamua kujiingiza kwenye muziki na alianza kusambaza ngoma zake kwenye redio kama Bagamoyo FM inayopatikana hapo Bagamoyo na baada ya muda akaamua kuingia jijini Dar Es salaam ili aweze kutimiza lengo lake la kuwa msanii mkubwa.
Baada ya kufika Dar es salaam, Mac Voice alifikia kwa mtoto wa shangazi yake aliyeishi huko Mbagala ambaye pia alikuwa anamsaidia nauli na pesa ndogo ndogo za kwenda kurekodi ngoma studio na kuna kipindi alishawishiwa na kaka yake huyo kwenda kufanya kazi gereji ili aweze kujikimu lakini alikataa kwani aliamini kwenye muziki na alianza kusambaza ngoma kwenye vituo mbalimbali vya redio.
Mac Voice alikutana vipi na Chege?
Wakati anafanya interview kwenye kipindi cha Lil Ommy kinachoitwa The Playlist, Chege alitaja ngoma ya Mac Voice ambaye kipindi hicho alikuwa ni msanii chipukizi kama moja ya ngoma anayoipenda na anayoisikiliza sana.
Baada ya kusikia taarifa hizo Mac Voice kama shukran kwa Chege aliweka video hiyo ya Chege akisifia ngoma yake kwenye ukurasa wake wa Instagram na ndipo hapo Chege alimfuata DM na kubadilishana namba za simu na wawili hao wakaanza kuwa na ukaribu wa kikazi na baada ya hapo akawa chini ya usimamizi wa lebo ya Unique Voice Music ya msanii Chege.
Chini ya UVM music Mac Voice alitoa ngoma tofauti tofauti na Chege kama vile "Damu Ya Ujana", "Mama J" pamoja na "Utarudi" ya mwaka 2019.
Mac Voice alikutanaje na Rayvanny?
Mac Voice alikuwa na ukaribu wa kikazi na Director Eris Mzava ambaye ndiye Director rasmi wa Rayvanny ambaye amehusika kuandaa video za muziki za Rayvanny kama vile "Jeniffer Remix", "Siri" na "Sugu".
Baada ya Eris Mzava kujenga ukaribu na Mac Voice, ndipo hapo Mzava alianza kumsikilizisha Rayvanny kazi za Mac Voice na Rayvanny alivutiwa haswa na kipaji cha msanii huyo hivyo akaomba kukutana na Mac Voice ili aweze kumfahamu zaidi.
Baada ya kukutana na Mac Voice, Rayvanny aliamini katika kipaji cha Mac Voice na aliahidi kumsaidia na ilipofika mwezi Septemba mwaka 2021 ndipo alimtambulisha msanii huyo mbele ya watanzania kwa mara ya kwanza.
Je Mac Voice ana albamu au EP?
Mac Voice ana EP moja inayoitwa "My Voice" ambayo imesheheni ngoma sita na ambazo ndani yake amemshirikisha bosi wake Rayvanny pamoja na Leon Lee kutokea nchini Afrika Kusini.
Nyimbo bora kutoka kwa Mac Voice
Nenda
Tamu ft Rayvanny
Nampenda ft Rayvanny
Pombe ft Rayvanny ft Leon Lee
Mama Mwenye Nyumba
Mahusiano ya Mac Voice
Kufikia sasa Mac Voice hajaweka wazi mahusiano kwenye vyombo vya habari au mitandao ya kijamii.
Leave your comment