Rayvanny Ashukuru Mashabiki Kwa Mapokezi Mazuri Waliompa Mac Voice

[Picha: Mac Voice Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii chipukizi kutoka Tanzania Mac Voice kwa muda sasa amekuwa akitawala anga za burudani kupitia EP yake ya 'My Voice' aliyoachia baada ya kutambulishwa kama msanii wa kwanza kusainiwa Next Level Music.

Mac Voice amepiga hatua kubwa sana katika taaluma yake ya muziki ndani ya muda mfupi. Ujio wake kwenye tasnia ya muziki kupitia lebo ya Next Level inayomilikiwa na Rayvanny umekuwa wa kipekee na wenye manufaa makubwa.

Soma Pia: Mac Voice Aeleza kwa Undani Alivyokutana na Rayvanny

Tayari Mac Voice amepata takwimu nzuri za idadi ya wafuasi katika mitandao mbali mbali ya kijamii. Kwa mfano kufikia sasa msanii huyo ako na zaidi ya wafuasi laki moja kwenye ukurasa wake wa Instagram. Kwenye mtandao wa YouTube ambao ndio msingi ya kila msanii, Mac Voice amefanikiwa kupata takriban wafuasi elfu tisini ndani ya takriban mwezi mmoja.

Bosi wa Next Level Music Rayvanny amewashukuru mashabiki kwa mapokezi mazuri ambayo walimpa Mac Voice. Chui, kama anavyofahamika kiusanii, aliendelea kwa kusheherekea mafanikio ya wimbo wa 'Nenda' kutoka kwa Mac Voice.

Ngoma hiyo iliyoachiwa mnamo tarehe 29 mwezi Septemba imepata takriban watazamaji milioni moja. 'Nenda' imeingia katika rekodi ya kuwa ngoma ya kwanza ya Mac Voice kutazamwa zaidi ya mara milioni moja.

Soma Pia: Mac Voice Asimulia Alivyohangaika kufanya Muziki Hadi Karibu Ajitoe Maisha

Aidha, Rayvanny aliashiria kupitia chapisho lake mtandaoni kuwa mafanikio ya Mac Voice yanatokana na yeye kufuata nyayo zake kwenye muziki.

"Like father like son @macvoice_tz Asanteni Kwa Mapokezi yenu makubwa kwa kijana wenu Imagine hata mwezi haujaisha," chapisho la Rayvanny kwenye ukurasa wa Instagram lilisomeka.

Leave your comment