Mac Voice Aeleza kwa Undani Alivyokutana na Rayvanny

[Picha: Bekaboy]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea lebo ya Next Level Music Mac Voice ameeleza kwa undani namna ambavyo aliweza kujenga mazoea na Rayvanny mpaka kutambulishwa kama msanii wa kwanza wa lebo hiyo.

Akiongea na chombo kimoja cha habari hapa nchini Tanzania,Mac Voice amedokeza kuwa alikutanishwa na Rayvanny kupitia Director Eris Mzava ambaye ndiye director rasmi wa Rayvanny.

Soma Pia: Mac Voice Aeleza Wosia Aliopewa na Diamond Kipindi Alijiunga na Next Level Music

Director Eris ndiye amehusika kuandaa video za muziki za Rayvanny kama ‘Teamo’ na ‘Valentine’.

"Mi nilikuwa nafanya kazi na Mzava, kupitia yeye Mzava ndipo Rayvanny akaniona. Mzava ni mtu ambae akipenda kitu anawasikilizisha watu sana kwa hiyo alikuwa anamsikilizisha sana Rayvanny ngoma zangu, nashukuru Mungu Rayvanny akawa anazikubali, kwa hiyo ya Mungu Mengi," alizungumza Mac Voice.

Soma Pia: Mac Voice Afunguka Kuhusu Maisha Magumu Yaliyomsukuma Kufanya muziki

Aidha katika mahojiano hayo, Mac Voice aliendelea kusisitiza kuwa yeye na msanii Chege ambaye alikuwa bosi wake kwenye lebo ya Unique Voice Music hawana ugomvi wowote.

"Sina ubaya wowote na brother Chege na Rayvanny ni mtu ambaye anamrespect sana Chege na ningekuwa na matatizo na Chege ina maana Rayvanny asingeweza kunisaidia. Chege ni brother wangu atabaki kuwa brother wangu. UVM na Next Level wote ni familia moja," alizungumza Mac Voice.

Kufikia sasa, Mac Voice ameshatoa video mbili ambazo ni ‘Nenda’ pamoja na ‘Tamu’ na zote zinapatikana kwenye EP yake yake ya ‘My Voice’  iliyoingia sokoni mwezi uliopita.

Leave your comment