Diamond, Rayvanny Watajwa Miongoni Mwa Wasanii Wa Afrika Waliotazamwa Zaidi YouTube 2021
31 January 2022
[Picha: All Africa]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Kutoka lebo ya WCB, wasanii Diamond Platnumz na Rayvanny wametajwa miongone mwa wasanii waliotazamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube barani kwa mwaka 2021.
Kwa mujibu wa ripoti ya YouTube ambayo iliainisha wasanii 10 kutoka Afrika hasa kusini mwa jangwa la Sahar, wasanii 7 kati ya 10 walitokea nchini Nigeria, mmoja nchini Congo huku Tanzania ikiwakilishwa na wasanii wawili ambao ni Diamond na Rayvanny.
Soma Pia: Lava Lava Adokeza Ujio wa Ngoma yake Mpya 'Desh Desh'
Diamond alishika namba tatu kwenye orodha hiyo kwa kutazamwa takribani mara Milioni 452 kwa mwaka 2021 pekee akitanguliwa na Wizkid aliyetazamwa takriban mara Milioni 576 huku namba moja ikishikiliwa na mkali wa ngoma ya ‘Love Nwatiti’ yaani Ckay ambaye alitazamwa takribani mara Bilioni 1.1 kwenye mtandao huo.
Kwa upandE wa Rayvanny alishika namba saba kwa kutazamwa takriban Milioni Milioni 266 huku akiwa amewazidi wasanii Fireboy DML na Omah Lay.
Soma Pia: Mbosso Atangaza Ujio wa Kolabo Tano za Kimataifa
Si jambo la kushangaza Rayvanny kuingia kwenye orodha hii kwani kwa mwaka jana aliweza kuachia kazi nyingi kwenye mtandao wa YouTube ikiwemo albamu yake ‘Sounds From Africa’. Pia alipakia video za muziki takriban 12 kwenye akaunti yake ya YouTube hivyo kupelekea kutazamwa zaidi.
Kando na rekodi hii, kufikia sasa bado Diamond Platnumz anashikilia rekodi ya kuwa msanii mwenye wafuatiliaji wengi zaidi kwenye mtandao wa YouTube barani Afrika kusini mwa jangwa la sahara.
Kwa sasa, Diamond ana wafuatiliaji takriban Milioni 6.1 akifuatiwa na Rayvanny mwenye wafuatiliaji takriban Milioni 3.5 kwenye mtandao huo.
Leave your comment