Mbosso Atangaza Ujio wa Kolabo Tano za Kimataifa

[Picha: Mbosso Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki wa bongo Mbosso ametangaza kuwa amekamilisha kolabo tano na wasanii wa kimataifa. Mbosso aliweka taarifa hiyo wazi kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Msanii huyo ambaye ni mwanachama wa lebo ya WCB alifuchua kuwa kwa siku za hivi karibuni alikuwa mjini Lagos, Naijeria ambako pia alikuwa akifanya kazi ya kimuziki.

Soma Pia: Lava Lava Adokeza Ujio wa Ngoma yake Mpya 'Desh Desh'

Aliwashukuru wadau tofauti wa muziki kutoka Lagos kwa mapokezi mazuri waliyompa. Baada ya ujumbe huo, Mbosso, vile vile, alichapisha picha za bendera ya taifa la Komoros, kuashiria kuwa huenda ameelekea huko au anafanya kazi ya kimuziki na wadau kutoka taifa hilo.

Mbosso hata hivyo hakutaja majina ya wasanii aliofanya kolabo nao au mataifa wanakotoka.

"Lagos has been real. The vibes and energy was crazy. I have 5 global hits. Hits collabos coming your way. Keep it locked here," ujumbe wa Mbosso mtandaoni ulisomeka.

Soma Pia: Whozu Atangaza Kuachia Albamu Mwaka Huu

Ikumbukwe kuwa mwaka jana, tuhuma ziliibuka mtandaoni kuhusu ujio wa kolabo baina ya Mbosso na msanii wa Kenya Mr. Seed. Hii ilikua baada ya picha zilizowaonyesha wawili hao wakiwa studioni kuvuja mtandaoni.

Kwa sasa, mashabiki wa Mbosso wamebaki na hamu kuhusu ujio wa kolabo hizo. Kwa mwaka huu, Mbosso ameacha kazi moja tu ambayo ni ‘Tausi’, aliyomshirikisha Mrisho Mpoto.

Kabla ya hapo, mwishoni mwaka jana aliachia ‘For You’ aliyomshirikisha Zuchu. Kazi zote zilipata mapokezi mazuri.

Leave your comment