Whozu Atangaza Kuachia Albamu Mwaka Huu

[Picha: Citi Muzik]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Whozu hatimae ametangaza kuwa ndani ya mwaka huu anatarajia kuachia albamu yake ya kwanza tangu aanze muziki.

Akiongea hivi karibuni kwenye kipindi cha Zege, Whozu amethibitisha kuwa ndani ya mwaka huu mashabiki watarajie albamu kutoka kwake japo hakuweza wazi tarehe ambayo albamu hiyo itaingia sokoni.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Ngoma Mpya ‘Mwaka Wangu’

"Albamu yangu inatoka mwaka huu siwezi sema direct ni mwezi gani na tarehe gani sababu ntakuwa natoka nje na makubaliano ya ofisi au management lakini itatoka mwaka huu na haitochelewa," alizingumza mtunzi huyo wa ngoma ya ‘Usinirekodi’.

Aidha, Whozu alidokeza kuwa kufikia sasa ameshafanya kazi na watayarishaji tofauti tofauti wa muziki, wote wakubwa kama S2kizzy na Mr Touch na pia amewapa nafasi watayarishaji wa muziki wadogo na wanaochipukia kuandaa albamu hiyo.

Soma Pia: Maua Sama Kumkaribisha Tanzania Msanii Dija Kutoka Nigeria

"Maproducer mnaoona nafanya nao kazi ni nafanya nao kazi ambayo direct iko moja kwa moja kwenye album. Yupo Touch yupo S2kizzy na wengine wengi wadogo wadogo wenye vipaji vya uprodyuza na walikuwa wanawishi kufanya kazi na mimi," alizungumza Whozu.

Kauli hii kutoka kwa Whozu imejibu kiu ya mashabiki kutaka kujua ni kazi gani hasa Whozu anaandaa kwani siku hizi za hivi karibuni kupitia akaunti yake ya Instagram amekuwa akionekana akirekodi ngoma studio akiwa na watayarishaji mbalimbali wa muziki kutokea Tanzania.

Kando na Whozu, wasanii wengine kutoka Tanzania wanaotarajiwa kuachia albamu mwaka huu ni pamoja na Diamond Platnumz, Ibraah, Young Lunya na Rosa Ree.

Leave your comment