Maua Sama Kumkaribisha Tanzania Msanii Dija Kutoka Nigeria

[Picha: EATV]

Mwandishi: Chatles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Maua Sama anatarajiwa kumkaribisha hapa nchini mwanamuziki kutokea nchini Nigeria Dija kwa ajili ya kufanya kazi ya pamoja.

Taarifa hizo zilitolewa hivi karibuni na mwanamuziki Dija ambaye kupitia akaunti yake ya Twitter aliandika kuwa amekaribishwa nchini Tanzania na Maua Sama hivyo panapo majaliwa anaweza kuwasili Tanzania.

Soma Pia: Maua Sama Atoa Kauli Yake Kuhusu Wasanii wa Bongo Kufanya Amapiano

"Tanzania soon we will be together inshaa Allah. Cc @MauaSama has invited me to come over!" aliandika Dija kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Mara baada ya chapisho hilo kutoka kwa Dija mashabiki wengi wa muziki wameshuku kuwa huenda ujio wa Dija nchini Tanzania ukapelekea wasanii hao wawili yaani Dija na Maua Sama kutoa ngoma ya pamoja.

Soma Pia: Maua Sama Aweka Wazi Mipango ya Kufungua Lebo Yake ya Muziki

Kwa upande wa Maua Sama huu ni mwaka ambao unaonekana kuwa bora sana kwake hasa upande wa kwenda kimataifa zaidi. Wiki moja iliyopita, Maua Sama alishiriki kwenye albamu ya ‘Man’ ya Fiokee kutokea nchini Nigeria, albamu ambayo pia wasanii wengine wakubwa kama Simi na Yemi Alade wameshiriki pia.

Dija ni nani?

Dija ni msanii kutokea nchini Nigeria ambaye alianza muziki mwaka 2008 na ilipofika mwaka 2014, mwanamuziki huyo ambaye ameshaishi Marekani, Nigeria, Sierra Leone na Canada alisainiwa na lebo ya Mavin ambayo inamilikiwa na Don Jazzy.

Kufikia sasa, ameshatoa ngoma zaidi ya 15 huku ngoma ya ‘Awww’ ya mwaka 2014 ikiwa ndo ngoma iliyompa mafanikio makubwa na kupelekea kujulikana zaidi barani Afrika.

Leave your comment