Maua Sama Atoa Kauli Yake Kuhusu Wasanii wa Bongo Kufanya Amapiano

[Picha: Maua Sama Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Malkia wa muziki wa bongo Maua Sama ametoa kauli yake kuhusu muziki wa Amapiano kutawala tasnia ya muziki wa Tanzania.

Kwa siku za hivi karibuni, mtindo wa Amapiano umepata mapokezi mazuri Afrika Mashariki huku wasanii wengi kutoka Tanzania wakiuiga mtindo huo. Idadi kubwa ya wasanii tajika Tanzania wametoa nyimbo za Amapiano ambazo zimepokelewa vizuri sana.

Soma Pia: Zuchu, Barnaba Wapinga Madai ya Muziki wa Bongo Kufa

Kando na kuibua mjadala mkubwa, wasanii wa bongo ambao hawajajihusisha na mtindo huo wamekodolewa macho mno na mashabiki. Mmoja wa wasanii hao ni Maua Sama ambaye alilazimika kutoa kauli yake kuhusu mtindo wa Amapiano.

Kwa upande wake, Maua Sama anaamini kuwa sio lazima kila msanii wa bongo kufanya muziki wa Amapiano. Alieleza kuwa hakuna anayelazimishwa kuimba kwa mtindo huo. Kwa mujibu wa msanii huyo, yeye anapenda nyimbo za bongo zaidi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: The Ben Aachia ‘Why’ Akimshirikisha Diamond Platinumz [Video]

"Kwani ikitokee hujaimbaAmapiano unaweza kufutiwa Cheti cha Usajili BASATA? Au utapokonywa NIDA & Passport? Nipo zangu sehemu hapa nakunywa soda naskiliza ZAI, UTU & I WISH (On Repeat) Nipo Airport njooni mnipige," chapisho la Maua Sama mtandani lilisomeka.

Kauli hiyo ilipata uungaji mkono kutoka kwa mfalme wa muziki wa bongo Alikiba. "Hakuna wa kukupiga ZAI wangu," Alikiba alimjibu Maua Sama.

Hapo awali Zuchu pamoja na msanii Barnaba Classic walijitokeza na kuwatetea wasanii wanaofanya mtindo wa Amapiano.

Leave your comment