Zuchu, Barnaba Wapinga Madai ya Muziki wa Bongo Kufa
3 January 2022
[Picha: Zuchu Instagram]
Mwandishi: Brian Sikulu
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Mabingwa wa muziki wa bongo Barnaba na Zuchu wamepinga vikali dhana ya kuwa muziki wa bongo umekufa.
Dhana hii ilitokana na kauli ya mchekeshaji kutoka Kenya Eric Omondi ambaye alidai kuwa wasanii wengi wa bongo wameingia kwenye mtindo wa Amapiano, na hivyo basi kufanya mtindo wa bongo kufifia.
Soma Pia: Harmonize ‘Serious Love’, Jay Melody ‘Sugar’ na Nyimbo Zingine Mpya Bongo Wiki Hii
Kupitia ukurasa wake wa kijamii, Zuchu alieleza kuwa muziki wa bongo kamwe hutowahi kufa. Aliwatetea wasanii wanaofanya mtindo wa Amapiano kwa kusisitiza kuwa wasanii hao wanajaribu mitindo tofauti ya muziki na kuonesha ustadi wao katika aina tofauti ya midundo.
Aliongeza kuwa ni jambo zuri wasanii wakijaribu mitindo mipya ili kuleta mabadiliko katika muziki.
"Bongo flavor can never die artists are going out of their comfort zones its called diversity. Trying new sounds has never killed any industry the music industry is big so let artists try out new things ndo mabadiliko hayo," chapisho la Zuchu mtandaoni lilisomeka.
Soma Pia: Ali Kiba Adokeza Kuachia Ngoma Mpya Mbili Hivi Karibuni
Kwa upande mwingine, Barnaba alisema kuwa mtindo wa bongo una nguvu kushinda amapiano.
"Nadhani Bado Bongo flavor Ina nguvu Sana kuliko Amapino Kingine lazima watu wajue Amapiano sio aina ya muziki Bali kwa lugha rahisi Ni mixing Za DJs wa SouthAfrIca wakiwa Kwenye gigs zao So haitaweza Kuuwa muziki halisi kama Rhumba Rege / Dans Pop Rock NK : kwa sababu sio haina ya muziki Bali ni vionjo to katika milindimo ya mziki," Barnaba alieleza.
Leave your comment