Harmonize ‘Serious Love’, Jay Melody ‘Sugar’ na Nyimbo Zingine Mpya Bongo Wiki Hii

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wiki ya kwanza ya mwezi Januari mwaka 2022 imeshawadia na wasanii kwenye kiwanda cha Bongo Fleva wameendelea kuachia ngoma kali ambazo kwa namna moja au nyingine zimezidi kunogesha mwaka huu. Zifuatazo ni ngoma mpya kutoka Tanzania kwa wiki hii.

Soma Pia: Amapiano Tano Kutoka Tanzania Zilizofanya Vizuri Zaidi Mwaka 2021

Cha Mbunge - Moni Centrozone ft Kusah

Huu ni wimbo ambao Moni Centrozone ameutoa kwa ajili ya wasichana warembo. Kwa kutumia kipaji chake cha kurap, Moni anamsifia mpenzi kwa namna anavyopendeza huku Kusah kwenye aya ya pili ya ngoma hii akitumia mdundo kutoka mtayarishaji wa muziki Trone kuweka mashahiri mazuri yanayozidi kupamba ngoma hii.

https://www.youtube.com/watch?v=qc-u5JnFXhE

Sugar - Jay Melody

Kama uliipenda ‘Sukari’ ya Zuchu basi bila shaka utaipenda ‘Sugar’ ya Jay Melody. Tangu kuachiwa kwake, ngoma hii imekuwa gumzo na kivutio hasa kwenye mtandao wa Tiktok kutokana na mashahiri yake ya, kuvutia pamoja na mdundo mzuri kutoka kwa Mocco Genius.

https://www.youtube.com/watch?v=A_lN45V3mbY

Soma Pia: Nyimbo Tano Zilizofanya Vizuri TikTok Kwa Mwaka 2021

Serious Love - Harmonize

Kutoka kwenye albamu yake ya High School, Harmonize ameachia rasmi video ya ngoma yake ya ‘Serious Love’ ambayo kwa kiasi kikubwa ameimba kwa lugha ya kiingereza chenye ya kinigeria huku video yake ikiwa imeelekezwa na Ivan. Kufikia sasa video hii imeshatazamwa mara laki mbili na elfu nane kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=59jN0K1n7ZM

Mbunge Anatucheka - Baba Levo

Baada ya kutikisa mwaka 2021 na Amapiano, Baba Levo anafungua 2022 na ngoma hii ya ‘Baba Anatucheka’ ambayo inagusia hasa masuala ya kisiasa ya namna ambavyo wabunge husaliti na kuwacheka wananchi pindi wapatapo madaraka kwa kutotimiza ahadi zao kipindi cha uchaguzi.

https://www.youtube.com/watch?v=kJo5-u-2YJs

Jamani - Country Wizzy

Ukiweka kando mashahiri ya ngoma hii ya ‘Jamani’ kutoka kwa Country ambayo yanazungumzia na kugusa maeneo tofauti tofauti ya kimaisha, kitu kingine kinachofanya ngoma hii kuwa bora ni mdundo wake wenye nguvu ambao ni mchanganyiko wa Jazz, Soul pamoja na Afro Beats.

https://www.youtube.com/watch?v=VvFfrqHtJPM

Leave your comment